NYIMBO ZA KUMUAGA RAIS JAKAYA KIKWETE HEWANI ! SI WENGINE NI NGOMA AFRICA BAND AKA FFU -Ughaibuni yenye maskani kule ujerumani 
 Mtunzi:Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja 
Waimbaji: Kamanda Ras Makunja Afande Chris-B ambaye pia ni mpiga solo gitaa Bendi: 
Ngoma Africa band aka FFU wasiliana nao at ngoma4U@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2015

    Kwanza hongereni sana ngoma africa band muziki huu umetulia na inaonekana nyinyi sio wezi wa fadhira sasa hapa bongo wanamuziki wote wamekuwa mdomo wazi
    wakisubiri mshiko wa wanaotangaza nia ya kugombea Urais 2015,lakini nyinyi mnahakikisha kwanza mnamaliza kazi na JK! kweli nyini ni wapiganaji msioyumba

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2015

    Burudani kubwa sana. Ni vizuri kutoa shukrani hasa kwa kuendeleza amani iliyokuwepo na kutuletea maendeleo ya miundo mbinu. "myonge myongeni lakini haki yake mpeni."

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2015

    hawa vichaa wanatisha sana duh! inaelekea wana timing sio ya kikawaida,kwa muziki wao sio wa kitoto ni muziki mkubwa mno,wametulia na inaonekana wanakijua wanacho kifanya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2015

    Sasa kazi naona kamanda Ras Makunja baada ya kupatikana kwa bundi wake aliyepotea sasa tunapata burudani, Kamanda mkuu huyu Ras Makunja na vijana wake anatisha sana tena anaonekana ni mzoefu kwa kurusha mistari inayogusa
    mioyo ya walio wengi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2015

    Mistari ya ujumbe huu inanitoa machozi kwa kuona kuwa baadhi yetu watanzania tumekuwa watu wenye kusahau leo hii wasanii
    wametekwa na kusubiri posho za vigogo wajao,lakini hapa naona hawa jamaa tena wapo mbali na nyumbani kwanza wanatoa shukurani kwa Kiongozi wetu ! Leo hii hapa nyumbani wapo wanamuziki wengi lakini wamesahau waliofanyiwa na JK

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2015

    Ankali Muhidin ,asante sana kwa huu muziki umeuibua wapi? ujumbe mzito sana wengi tumeguswa na maneno ya waimbaji wamemshukuru mpaka mama 1st lady kwa uvumilivu,wamewashukuru wazaa chema wazee wa msoga kwa malezi bora na kumsomesha JK,wanasema La Mgambo limelia JK anamaliza kazi wakati taifa bado lina muhitaji ,wimbo huu unanitingisha hisia na machozi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2015

    Huyu mtunzi sio kiumbe au binadamu wa kawaida mistari yake ukisiliza ina choma na kupuliza anasema "nyinyi mlio mbali na mlio karibu njooni muone nchi JK kafanya mengi" yaani anawafumbua macho wanaojifanya vipofu !

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2015

    Michuzi unajua hawa jamaa sio wanamuziki wa kawaida kuna kipande kimesikika
    kwa mistari "Mnyonge Mnyongeni haki yake Mpeni" mtunzi ni mswahili kweli
    anawachana Live wasio na shukurani,mtunzi anasimama kwa kulinda yote yaliofanywa na JK,kuwa watanzania tunabudi ya kutoa asante sio kukimbilia posho za watangaza nia

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2015

    Yes nakubali anko mtandao wako sio mdogo umewafungulia watoto wa mbwa sasa wanabwaka kweli umeshalileta baraa unawasikia mdundo wao machizi hawa ni tofouti sana na muziki wa kitoto wa katika computer,yaani waimbaji wapo katika key wametulia na ukiwa mwimbaji mtoto upenyi hata kidogo hapo-Asante sana kwa kuleta vitu adimu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2015

    Mguu upande Mguu Sawa Kamanda ras makunja anaongoza gwalide la ffu,imebidi nisikilize na kucheka tu,maana machizi wa muziki ngoma africa hizi ndizo zao
    nimeona wanamuziki wenzao wapo Dodoma wakionyesha nini walichokifuata kule
    huku kumbe Kamanda wa ffu anatangaza La Mgambo na kuvipa kazi vituo vya redio

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2015

    Kweli kazi hipo huu wimbo niliusikia ghafla katika kituo cha Zenj FM leo jioni kama x2 hivi ukichezwa na kutufanya wasikilizaji wa hapa Unguja katika maeneo ya darajani kusimama kama vile tumenaswa na umeme ,sio ngoma ya kitoto

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2015

    kama ni tuzo basi wanamuziki hawa ndio wa kupewa,si amini masikio na macho yangu kuwa wanamuziki wapo mbali sana na nyumbani na wakatoa kitu kizito kama hii ngoma respect

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2015

    aaaaaahaaahah nina wasiwasi na hizo comment zote hapo juu!! ni shiiiiiiiiidah

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 11, 2015

    du jamani mimi sina chama nipo canada nimerudi tanzania nimeona sio ile niliyoiacha kikwete kafanya kazi tuache unafiki kama binadamu anamapungufu yake ila kafanya kazi huyu dude.waliomharibia ni watu aliyokuwa akiwateua akizani watafanya kazi kumbe niwadaka tonge,
    sasa hawa akina ras ndio wanamuziki du wamenikuna hawa dude mmh,
    vielen dank

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 12, 2015

    jk jembe tutake tusitake nchi imebadilika jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...