Na Bashir
Yakub
Wiki kadhaa zilizopita
nilipigiwa simu na
mama mmoja akitaka
nimpe ushauri wa
sheria kuhusu jambo
fulani. Nilifanya miadi naye
na tukafanya mazungumzo.
Kubwa kuhusu shida
yake ilikuwa ni
tatizo la mkopo ambapo
benki moja imeuza nyumba
yake maeneo ya
Kinondoni Dar es
saaam. Wasiwasi wake
ulikuwa ukiukwaji wa
taratibu za mauzo
ya nyumba yake na
hivyo akitaka kujua
afanye nini. Maswali yake
yalikuwa mengi na
nilimjibu kwa kiwango
cha juu.
Pamoja na hayo
kilichokuwa kikimpa shida sana na
kuamini kuwa kulikuwa
na mchezo mchafu
umefanyika katika uuzwaji
wa nyumba yake ilikuwa
ni hatua ya benki
inayomdai kujiuzia nyumba
yake katika mnada
wa hadhara. Alidai hakuwahi
kuona mdai deni
anajiuzia mali iliyowekwa kwake kama dhamana.
Alidai anavyojua ni
mnada kutangazwa na
wenye nia hujitokeza
kununua na kati
ya hao mdai
hawezi kuwa mnunuzi.
Aliamini hatua ya
mdai kuwa ndiye
mnunuzi ulikuwa ni
mchezo uliopangwa ili
kuchukua nyumba yake. Nilimuuliza
kilichomuudhi zaidi nini
kwani sioni tofauti
kati ya mtoa
mkopo kujiuzia mwenyewe na
kununua mtu mwingine
kwani kuuza ni
kuuza tu.
Akanieleza ukweli
kuwa wao walishampanga ndugu yao
ambaye angeweza kununua
na kwakuwa ni ndugu kuna
mipango yao kama
familia walishaipanga. Kwa
hiyo alihisi ilifanyika
hila ili wao
wasiichukue tena nyumba
hiyo kwakuwa mdai
naye alikuwa akiitaka kwa
udi na uvumba . Nilimpa ushauri
ambao ningependa pia
kuushiriki na watu
wengine kupitia makala
haya ili faida iwe kubwa. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...