Na Bashir Yakub
Makala zilizopita nilieleza mazingira ya kisheria ambapo mtu anaweza kunyanganywa ardhi yake na kufutiwa hati miliki na hatimye ardhi kupewa mtu mwingine au kukabidhiwa mikononi mwa serikali. Nilieleza mambo mengi ikiwemo sababu ambazo zinaweza kupelekea mamlaka za ardhi kufuta hati miliki ya mtu.
Pia nilionya kuwa unapomiliki ardhi sio kwamba umemaliza, hapana, isipokuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia na kufuata masharti yaliyo katika hati miliki. Hii ni kwasababu Sheria ya Ardhi imeweka bayana na kutoa mamlaka kwa ofisi kuu za ardhi kufuta umiliki wa mtu iwapo unakiuka masharti ya hati.
Pia nikaeleza kuwa yawezekana maafisa ardhi kutumia mwanya huo kuchukua ardhi yako kwa manufaa fulani au kwakuwa yupo mtu nyuma ya mchezo huo ambaye anaitaka ardhi yako.
Utatumika mwanya wa kutotekeleza masharti kukunyanganya ardhi ili apewe huyo aliyesimamia mchezo huo. Na mwisho nikasema kuwa huwezi kujua kama haya yapo mpaka yakutokee vinginevyo unaweza kudhani tunaongea vitu ambavyo havijawahi kutokea. Waliofikwa na haya wanajua nazungumza nini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...