Mhandisi mashuhuri George Mulamula,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi),  (pichani) ameipongeza programu mpya ya Airtel Tanzania  ijulikanayo kama  “Airtel Fursa” inayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli zao. 
Kama mmoja wa jopo la washauri ambaye atachagua  vijana watakaotimiza vigezo vya kuweza kuingia katika mpango wa Airtel Fursa. 

"Hii ni nafasi nzuri  ya kuleta mabadiliko, kuhamasisha vijana na kuwasaidia kujijenga kibiashara endelevu na ninapenda kuwapongeza Airtel kwa ajili ya mpango huu," alisema Mulamula. 
Bwana Mulamula aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Airtel pamoja na jopo la washauri  katika kuhakikisha wanachagua na kuwapa mafunzo walengwa wa Airtel Fursa  ikiwa ni pamoja na kuwasaidia  kuweza kutumia techonologia ya habari yaani ICT kama nyenzo  muhimu itakayowawezesha kuleta ufanisi katika shughuli zao za uzalishaji na kiuchumi.  Akiamini kuwa vijana watakaofaidiaka na Airtel fulsa watahamasisha na kuongoza katika kuleta mabadiiko kwenye jamii zao huku akihakikisha mpango huu unakuwa na mafanikio makubwa kwa walengwa  na kuwa na mvuto kwa vijana wengine . 
Mhandisi Mulamula ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi) kwa ajili ya ujasiriamali katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), analeta uzoefu wa kutosha katika mpango huu  wa Airtel fursa kwenye nyanja ya  ujasiriamali na kukuza biashara zinazoanza. 
Yeye ni mshauri na mwalimu kwa wajasiriamali. Amekuwa akisaidia kuinua vipaji vya watu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali nchini Moscow, Durban na Nairobi kwa ajili ya maonyesho ya Afrika. Pia ni Mjumbe wa Bodi ya Demeter nchini Boston USA na pia Mjumbe wa Bodi ya XPrize nje ya California, Marekani. 
“Mpango huu unatafuta vijana wenye kiu, nguvu na utayari wakupata wanachokiamini na kukihitaji, wenye uwezo wa kuzipitia changamoto na kufikia matarajio waliojiwekea na wakati huohuo kubadilisha maisha yao” aliongeza 
Airtel Fursa inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao ni watanzania waishio nchini Tanzania. Vijana hao ni lazima wawe wamiliki wa biashara ndogondogo, wenye hali ya ushindani na kuheshimu biashara zao. Maelfu ya vijana watapata mafunzo kupitia warsha mbalimbali na kupatiwa vitendea kazi vitakavyo boresha biashara zao.
 Hii inajumuisha mafunzo katika usimamizi wa fedha, mikopo, faida za kuwa na akaunti ya benki na usimamizi wa biashara kwa ujumla 
Wanaotaka kujiunga wanapaswa kutuma ujumbe mfupi kwenda 15626 ukiambatanishwa na taarifa zifuatazo;- jina, umri,aina ya biashara, mahali na namba ya simu. Airtel Fursa pia inakaribisha mapendekezo ya vijana wenye vigezo husika. 
Maombi yanaweza kutumwa pia kwa njia ya barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com  au tovuti ya Airtel. Maombi yaambatanishwe na jina, umri, aina ya biashara, mahali, namba ya simu na sababu ya kusaidiwa kibiashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2015

    Sekta binafsi inapoweza isaidie vijana wetu kuendeleza biashara zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...