MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Zoezi hilo lilo anza majira ya saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.

Akizungumza katika eneo hilo Mhe. Nassari alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika ugali na kazi ikaendelea”alisema Mhe.Nassari.
Mhe. Nassari aliwashukuru vijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.
Mhe. Nassari aliwashukuru vijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.
![]() |
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Mhe Joshua Nassari akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. |
![]() |
Mbunge Nassari akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Dah Dogo anajitahidi sana kushiriki shughuli za kijamii... Hongera Mh...
ReplyDeleteJamani, Mbunge kudandia Lori tena ina husu? let us be realistic and not pretending, kwanza anahatarisha maisha yake, likifeli break itakuwaje hapo. I am just thinking aloud!
ReplyDeleteHuyu ni mbunge asiejielewa na vilevile kupotosha jamii kuhusu usalama. Hebu fikirieni mbunge kadandia lori je,mtu ambaye hana elimu kabisa ya usalama si atadandia kwenye tairi.wewe nasari ni mfano mbaya sana kwa jamii
ReplyDelete