Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Ali akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua mpango wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa,
2. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Raphael Mwamoto, akitoa maelezo kuhusu mpango wa Madaktari Bingwa wanaopelekwa mikoani na Mfuko huo.
Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakisubiri huduma za madaktari Bingwa,
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Fatma Ali akiwa katika picha ya pamoja na madaktari Bingwa baada ya kuzindua rasmi huduma ya madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara,
..........................................................................................................
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF unaendelea na mpango wake wa kupeleka madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa.
Mpango huo pia unalenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko katika hospitali za mikoani ambao watafanya kazi pamoja na madaktari bingwa hao.
Madaktari waliokwenda Mtwara ni pamoja na wagonjwa ya akinamama,m magonjwa ya ndani, bingwa wa upasuaji na bingwa wa dawa za usingizi.
Zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku sita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...