MKUU WA MKOA WA LINDI MWANTUMU MAHIZA AKIWASISITIZA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA WANAWAKE LILILOWAKUTANISHA TAKRIBANI WASHIRIKI WANAWAKE 360 KUTOKA WILAYA 6 ZA ,KUTUMIA MAFUNZO HAYO KUJIKWAMUA KIUCHUMI KWANI MIONGONI MWA WALIYOFUNDISHWA,UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI,KILIMO CHA MWANI NA MENGINEYO AMBAPO PIA KWA KUONYESHA DHAMIRA YA DHATI YA KUMKOMBOA MWANAMKE KIFIKRA NA KIUCHUMI ALIWATAKA KUHAKIKISHA WANAJIUNGA CHF ILI WAWEZE KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU KWA GHARAMA NAFUU,KAULI MBIU YA MAFUNZO HAYO IKIWA..MWANAMKE ANAWEZA KAMATIA FURSA..KONGAMANO HILO LILIFANYIKA HIVI KARIBUNI KWENYE SEKONDARI YA ILULU WILAYANI KILWA.
WASHIRIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI RAI YA MKUU WA MKOA WA LINDI MWANTUMU MAHIZA KWENYE KONGAMANO HILO.
MENEJA MWANDAMIZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA GRACE LOBULU AKITOA ELIMU YA MPANGO WA KIKOA UNAOWAHUSU ZAIDI WANAVIKUNDI WALIOSAJILIWA KAMA VILE VIKOBA,WAJASIRIAMALI NA SACCOS,KUCHANGIA HUDUMA ZA MATIBABU KWA GHARAMA NAFUU YA SHS.76800 MARA MOJA KWA MWAKA MZIMA,KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE WA MKOA WA LINDI LILILOKUWA NA LENGO LA KUWAJENGEA UWEZO WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KUTOKANA NA FURSA ZILIZOPO MKOANI HUMO,PIA ALIWASISITIZA KUWA MABALOZI WA MFUKO KATIKA KUFIKISHA ELIMU HIYO KWA WANAWAKE WENZAO. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2015

    Ni vuziri wanawake kujikwamua kiuchumi, ili muweze kumudu maisha ya nyakati hizi. Mmepatiwa mafunzo sasa kazi kwenu mchakarike.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...