Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo .
Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi.
Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika mikoa aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima, wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi.
Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi akizungumza katika kikao hicho kilichowashirikisha watendaji wa mkoa wa Iringa.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...