
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ofisi za Wizara hiyo, Mkurugenzi wa MAELEZO Assah
Mwambene,(Pichani) aliwataka wananchi kuitumia tovuti hiyo kupitia anuani ya www.wananchi.go.tz kuwasilisha hoja zao
Serikalini ili ziweze kupatiwa majibu .
“Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari- MAELEZO, imekamilisha
kufanya maboresho ya tovuti ijulikanayo
kwa jina la Tovuti ya Wananchi” alisema Mwambene na kuongeza:
“Lengo letu
sasa ni kutaka wananchi badala ya kuhangaika sana, akiwa sehemu yoyote ya nchi
hii anaweza kuuliza swali kupitia mtandao wa intaneti kwa anuani ya www.wananchi.go.tz”
Alisema mwananchi
akiingia kwenye tovuti hiyo atakutana na sehemu ya kuweka hoja yake kuuliza
swali, kutoa maoni, kutoa pongezi, kuwasilisha malalamiko yake na moja kwa moja
yatapokelewa na MAELEZO na kufanyiwa kazi.
“Mwananchi
anaweza kuandika swali moja kwa moja kwenye taasisi anayotaka swali lile liende,
kwa mfano kama anataka swali lile liende Wizara ya Ardhi anaweza akaandika”
alisema Mwambene na kuongeza:
“Sisi
tutapata taarifa kwamba ameleta swali na tutalipeleka kwenye taasisi husika na
tutaangalia na kuona je swali hilo limejibiwa ama halijajibiwa”.
Mwambene
alifafanua kuwa kila siku MAELEZO itajua ni wizara gani ama taasisi gani ya
Serikali imepelekewa swali gani na swali hilo limejibiwa au la.
Alisema
tovuti hiyo ni chombo muhimu katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia na
itamfanya mwananchi asilazimike kutembea kutoka kwenda wizara moja hadi nyingne
ama taasisi ya Serikali kushughulikia malalamiko yake.
Alitoa mfano
kuwa hata mwananchi akitaka kujua jinsi ya kupata viza au huduma nyingine
inayotolewa na Serikali ataweza kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi sana
kupitia tovuti hiyo ya Wananchi.
“Baadaye
kuna jambo lingine ambalo bado tunalifanyia tathimini, ni suala la kwamba wanaanchi
wanaweza kutumia simu zao za mkononi kutuma maswali na kupokea majibu” alisema
Mwambene.
Alibainisha
kuwa tathimini hiyo ikikamilika hivi karibuni, watatoa namba ambayo mwananchi
anaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mokononi kutuma hoja yake Serikalini na
kupatiwa majibu kupitia njia hiyo.
“Ni tovuti
ambayo tunapenda wananchi waitumie ili kupunguza gharama na muda mwingi sana
kwa mfano mtu kusafiri, kupanda gari kwenda wizarani au taasisi ya umma kufuatilia
shida yake.Hivyo anaweza kutumia simu yake ya mkononi” alisema Mwambene na
kuongeza:
“Lengo letu ni
kwamba wananchi waone kama hiyo ni fursa muhimu ya mawasiliano na waone kuwa
sasa hivi wanaweza kutuandikia ujumbe kuuliza swali au malalamiko na yatatufikia
na kufanyiwa kazi”.
Mwambene
alisema Wizara imejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba Serikali inawasiliana
na wananchi wake kwa kusikiliza shida zao na kuzipatia majibu.
“Hii ni Serikali
ya wananchi na lazima tuwasiliane na wananchi kwa njia yoyote ambayo ni rahisi
kuwafikia na Serikali imeona hii ni njia rahisi zaidi kuwafikia kupitia mtandao
huu wa Tovuti ya Wananchi” alisema.
Tovuti ya
Wananchi imewahi kufanya kazi katika miaka iliyopita na baadaye ilisimama
lakini sasa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo imeifanyia marekebisho makubwa na iko hewani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...