Meneja uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando akiongea na mshindi
aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya wiki ya
promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel
kutoka mikoa ya Geita na Mtwara walipatikana akichukua taarifa za
mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha
bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana
Fabian Felician.(kati) droo hii imechezwa leo katika makao makuu ya
Airtel Moroco jijini Dar es saalam.
aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya wiki ya
promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel
kutoka mikoa ya Geita na Mtwara walipatikana akichukua taarifa za
mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha
bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana
Fabian Felician.(kati) droo hii imechezwa leo katika makao makuu ya
Airtel Moroco jijini Dar es saalam.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel
imechezesha droo ya kwanza ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko"
nakutangaza washindi wawili wa kwanza wa wiki waliojishindia kila
mmoja pesa taslimu.
Akiongea kuhusu droo ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel
Bwana Jackson Mmbando alisema"Promosheni ya "Jiongeze na Mshiko"
itawawezesha watanzania kujinga na kushiriki bure na kupata nafasi ya
kujishindia shilingi milioni moja kila wiki na mwisho wa promosheni
kujishindia milioni mbili. Lakini mteja anawea kuamua kujiongeza na
kushiriki kwa tozo ya shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya
kujishindia zawadi nono zaidi ikiwa ni pesa taslimu shilingi milion 3
kila wiki na mwisho wa promosheni mteja ataweza kujindia milioni 50.
Akitangaza washindi Mmbando alisema" Leo tumechezesha droo ya wiki ya
kwanza tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" wiki
iliyopita. Ninayo furaha kutangaza washindi ambao ni pamoja na
Plasikus Gabriel Balimasu (25) Mlinzi na mkazi wa wa Mkoa wa Geita
yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na mshindi wa pili ni Rashidi
Hassan Mshabaha (27) mfanya biashara ndogondogo na mkazi wa mkoa wa
Mtwara yeye amejishindi shilingi milioni 1.
"Tunaamini ushindi huu utawawezesha wateja wetu kupata fedha za
kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kuboresha maisha yao, hilo ndilo
lenge letu kama Airtel kupitia kampaini yetu ya"its now" inayolenga
kuwawezesha na kuwainua watanzania kuzifikia ndoto zao. Natoa wito
kwa watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma ujumbe wenye neno
BURE kwenda namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia droo
zetu za kila wiki." aliongeza Mmbando.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...