TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imefuturisha wadau wake wanaoendelea na mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, huku ikiwataka kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala wa Bayport Financial Services, Evelyine Hall, katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wadau wake mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.


Viongozi wa Taasisi ya Bayport Financial Services na wageni waalikwa wakijadiliana jambo katika futari ya Bayport iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza wa tatu kutoka kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, mara baada ya kumaliza kufuturu katika futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Wilaya Kilwa, DC Abdallah Ulega kulia, akipiga picha na Meneja Utawala wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Evelyine Hall na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto. DC alikuwa miongoni mwa wadau walioalikwa katika tukio la futari lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mambo ya mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...