Jamii yashauriwa kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye shida mbalimbali hasa wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatima ili waweze kujisikia wanaishi sawa na watu wengine.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Allen Nyumbo wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa niaba ya Taasisi yao ya Vodacom Foundation kwa wazee kutoka kaya 65 za kijiji cha Mnimbila katika jimbo la Mtama jana.
Nyumbo alisema kuwa matatizo ya wazee, walemavu, na watoto yatima yanahitaji kutatuliwa na watu wenye moyo wa huruma ambao wanaguswa na shida za makundi hayo,hivyo ni vyema kila Mtanzania na mashirika mbalimbali yakaona umuhimu wa kusaidia makundi hayo ambayo yanajiona na kuisi yametengwa.
Alisema Vodacoma Foundation imeona umuhimu wa kusaidia chakula, mchele, sukari, unga wa mahindi, mafuta ya kula natende katika kaya hizi zilizopo Lindi, Kigoma, Rufiji, pamoja na Dar es salam baada ya kusukumwa na kuona umuhimu wa makundi hayo katika jamii.
Akizungumza kwania ya wakazi wa kijiji hicho Sophia Nyamanzi alisema msaada huo umewafikia katika wakati mzuri kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula hali ambayo inawafanya kushindwa kumudu hata kufuturu kwa msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Nyamanzi alisema kuwa mahitaji yao ni makubwa lakini msaada hao umepunguza kiasi cha shida zao walizokuwa wanazikabili kwa wakati huu ila wanaomba watu wengine wanaokuguswa na familia kama zao kuiga mfano wa Vodacom Foundation ili waweze kuwasaidia.
Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Lindi, Allen Nyumbo(watatu toka kushoto) akimkabidhi Mzee Selemani Musa Mkazi wa Lindi kapu lenye vyakula mbalimbali kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.
Sophia Nyamazi kazi wa kijiji cha Mnimbila Lindi Mkoa wa Pwani(kulkia)pamoja na wenzake wakipokea kapu lenye vyakula mbalimbali toka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani ikiwa ni kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.
Mkazi wa Lindi Mkoa wa Pwani Aisha Saleh(wane toka kushoto)akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali toka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani ikiwa ni kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.
Ustaadh Mwakifulefule sijamuona kwenye Mwezi huu Mtukufu!
ReplyDelete