Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa nchi zilizoendelea ndio zinaongoza katika
uharibifu wa mazingira kwa utumiaji wa Nuklia ,pamoja na uchimbaji wa Chuma hivyo
zinawajibu kuwekeza katika mabadiliko tabia nchi kutokana na kuchangia hali
hiyo .
Hayo ameyasema leo Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia
Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga wakati wa matembezi ya amani ya Mabadiliko
ya Tabia ya Nchi yaliyofanyika viwanja vya
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamezidi kukua kwa kasi
kutokana na uharibuifu wa mzingira unaofanywa na binadamu kwa shughuli za kila
siku huku jitihada za kukabili
mabadiliko hayo zikichukua asilimia ndogo.
Mwanga amesema malengo 17 ya maendeleo endelevu ya tabia ya nchi
ya mwaka 2015 -2030 kunahitaji viongozi kushughulikia katika
vyanzo mbalimbali vya fedha katika kuweza kufikia malengo na kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara
ya ukame,njaa, vifo pamoja na mafuriko.
Aidha amesema kuna mikutano mbalimbali inakuja hivyo ni kila
mtu kwa nafasi yake ashiriki katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi
katika nchi iweze kuwa na uchumi imara.
Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegeme wakihamasisha urtunzaji wa mazingira katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee ya jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango mbalimbali yenye jumbe tofautitofauti ili kuhamasisha yamii kuachana na uchafuzi wa mazingira ili kuokoa maisha ya watanzania kutokana na kuwa na majamba mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi
yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam leo.
Mratibu
wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga akizungumza na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi mara baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja ya wadau mbalimbali wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa na mabango ambayo yanahamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na ujumbe wa kuokoa maisha ya jamii kwa kutunza mazingira, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi
yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...