3Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu burudani hii adimu! Sasa utamu umewadia!!

Msimu wa pili wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup chini ya udhamini wa Dr. Mwaka, Daktari bingwa wa masuala ya Afya ya uzazi na Tiba asilia kutoka kituo cha Foreplan Clinic, kilichopo Bungoni, Ilala, Dar es salaam umezinduliwa rasmi katika uwanja wa Bandari, Tandika, jijini Dar es salaam.

Mechi ya ufunguzi yenye mvuto wa aina yake imepigwa jana ikiwakutanisha mabingwa watetezi, Abajalo FC ya Sinza Dar es salaam dhidi ya timu iliyojizolea Umaarufu ya wauza mitumba wa Tandika, FC Kauzu na hadi dakika 90 zinamalizika wanaume hao wa ‘Shoka’ walitoka suluhu (0-0).
5Sports Xtra Ndondo Cup ni mashindano yenye heshima kubwa kwa sasa na kwa kulitambulia hilo, Mgeni rasmi alialikwa kufungua pazia ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha mkoa wa Dar es salaam, Wilfred Kidau akiambatana na mwenyekiti wa chama cha soka cha Dar es salaam (DRFA), Almas Kasongo pamoja na mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA), Peter Muhinzi.
2Kwa wale ambao hawakushuhudia!, hakika mechi ya ufunguzi ilikuwa nzuri mno ikichagizwa na wachezaji wa ligi kuu wanaokipiga katika michuano hayo, mfano FC Kauzu walimtumia mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Atupele Green na ngome ya ulinzi iliongozwa na beki wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.
7Cha kufurahisha! FC Kauzu wanatumia jezi za Zambarao kama ilivyo kwa Mbeya City FC, hivyo Nyosso alionekana kama anakipiga katika kikosi hicho cha Juma Mwambusi. Abajalo FC wao walikuwa na mtu kama Paul Maona na nahodha wao George Kavila wanaokipiga Kagera.
8
Mashabiki zaidi ya Elfu tano walihudhuria mechi hiyo iliyojaa vitimbwi, mbembwe za kila aina na nimekuwekea baadhi ya picha zikionesha shamrashamra za mashabiki wa Sports Xtra Ndondo Cup Chini ya udhamini wa Dr. Mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...