Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. George Fumbuka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi. Ameambatana na Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo Bw. Jonathan Swalala (Kulia) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician (kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT). 
Meneja uendeshaji wa kampuni ya Core Securities Limited, Bw. Jonathan Swalala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Umande Unit Trust (UTT), mfuko wa uwekezaji wa pamoja utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi. Ameambatana na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. George Fumbuka (wa pili kushoto) na Meneja Mahusiano ya Wawekezaji, Bi. Sandra Felician (kushoto). UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT).

Kampuni ya Core Capital Securities imezindua mfuko wa uwekezaji wa pamoja uitwao Umande Unit Trust, utakaowawezesha wakezaji wengi kukusanya mitaji yao kwa pamoja ili kupata mtaji mkubwa zaidi.

UUT ni mfuko wa pili wa pamoja kusajiliwa nchini, kufuatia mfuko ulio chini ya serikali unaojulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa UUT Bw. George Fumbuka alisema kuwa wawekezaji wamepatiwa njia nyingine iliyo salama na rahisi zaidi itakayowawezesha kuwekeza fedha zao.

“Faida ya uwekezaji hutokana na ukubwa wake, yaani mtaji mkubwa huzaa faida kubwa zaidi. Lakini pia hutokana na kusambazwa kwake katika mirija kadha wa kadha ya uwekezaji,” alisema.

“Mwekezaji akitukabidhi mtaji wake, fedha huwekezwa katika mipango mikubwa ambayo mwekezaji mmoja mmoja asingeweza kuifikia. Ni wakati umefika watanzania wachangamkie fursa hii ya uwekezaj wa pamoja ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini,” alifafanua.

Bw. Fumbuka alisema kuwa mfuko huo utawekeza katika mafungu matatu lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya watu kutoka kwenye makundi mbalimbali.

“Fungu la kwanza litajulikana kama Umande Capitalisation Fund, fungu hili litawafaa vijana na wafanyakazi wanaotaka kufaidika na kukua kwa mtaji wao kulingana na soko la hisa. Katika fungu hili, asilimia 95 zitawekezwa katika hisa za makampuni yenye dalili nzuri ya kukua na asilimia tano iliyobaki itawekezwa katika amana za muda mfupi zenye kuzalisha riba nzuri,” alibainisha.

Aliongeza kuwa fungu la pili ni Umande income Fund linalowafaa wanaotaka usalama wa mitaji yao huku wakipata faida ya kutosha ambapo asilimia 75 zitawekezwa katika dhamana za serikali na asilimia 25 katika hisa ili kupata faida itokanayo na kukua kwa soko la hisa la Dar es Salaam.

Alisema kuwa fungu la tatu linajulikana kama Umande Balanced Fund ambapo asilimia 60 itawekezwa kwenye hisa za makampuni na asilimia 40 kwenye dhamana za serikali na mabenki. Alisema kuwa ofa ilifunguliwa tarehe 18 Mei 2015 na Itakamilika 24 Julai 2015, ambapo katika kipindi hicho kila kipande kitauzwa kwa shilingi 100.

“Tunatarajia vipande vianze kuuzwa au kununuliwa kutoka kwa meneja mnamo 27 Julai 2015. Tukiwa tunasonga mbele, UUT tumejipanga kutambulisha bidhaa na huduma bora zaidi katika soko lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya makundi tofauti tofauti katika jamii,” alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2015

    Utaratibu wa kununua vipande ukoje?
    Ofisi zao zipo wapi?
    UUT inatofautiana vipi na UTT?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...