Katibu
wa vijana umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji
akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za
umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata
nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha(Habari Picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog).
Mgombea
ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa leo amechukua fomu
ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema
kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya
ajira.
Neema
ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa
ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo
endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta
maendeleo katika Mkoa wa Arushaa .
Pia
mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake anayempa ushirikiano mkubwa
wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume
wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya
kuwania nafasi za uongozi.
Kwa
upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji
amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua
fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa
Arusha.
Khimji
alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni
kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama
hicho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...