Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni,yenye makao nchini Ujerumani,inatarijiwa kutumbuiza katika maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni Mamling Festival siku ya jumapili 5 Julai 2015 alhasiri katika viwanja vya Schlosspark,Mamling 3, Mining nchini Austria.
Watayarishaji wa onyesho hilo wameitaja bendi hiyo ya Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu unawapeleka puta washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini Austria wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima.
Kikosi kazi hiko chenye tabia ya kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki lukuki kote duniani,kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria.
Ziara ya bendi hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya wanamuziki wapo katika swaumu lakini
watatekeleza wajibu wao.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja ni bendi iliyobatizwa majina mengi ya kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama FFU-Ughaibuni, "Watoto wa Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien' na mengi mengineyo. ni bendi yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbili
mpya katika CD " La Mgambo" za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda.
Sikiliza at
wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni tayari kwa rigwaride
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni wakipiga kwata
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni ni balaa
Varangati likithibitiwa na FFU ughaibuni
ffu-ughaibuni mpaka sasa ndio kikosi pekee cha kiafrika ughaibuni chenye kuwa na washabiki wa mataifa mbali mbali,hongereni sana
ReplyDeleteVichaa nawakubali kazi wanaiweza ya kuthibiti vagaranti
ReplyDeletewatoto wa mbwa aka ffu chini ya kamanda aliyepindia akili rigwaride ras makunja kufanya naye kazi inataka uwe mjeshi
ReplyDelete