·
ORIGINAL KOMEDI WAWA
KIVUTIO
Siku ya PSPF
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF ilifana na kuvutia mamia ya wananchi
waliotembelea maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam
yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Siku
hiyo ni maaluma kwa ajili ya kutoa elimu ya Mfuko wa PSPF kwa umma ili waweze
kupata uelewa mpana wa sekta ya Hifadhi ya Jamii hususan bidhaa na huduma
zinazotolewa na PSPF, kwa mwaka huu, PSPF ililenga kuhimiza watanzania kujiunga
na Hifadhi ya Jamii kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari unaoendeshwa na PSPF.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizipo zaidi ya asilimia 90 ya watanzania hawapo katika
Hifadhi ya Jamii, hivyo jukumu kubwa la siku
ya PSPF mwaka huu ni kuhakikisha
watanzania wengi wanajiunga na PSPF, jambo hilo lilifanikiwa kwani zaidi ya
watu 500 walijiunga na PSPF katika maonesho ya sabasaba ya mwaka huu.
Siku
hiyo ilitumika kuwahamasisha wanachama wa PSPF kuwa na utaratibu wa kuhakiki
taarifa zao mbalimbali ikiwawemo, historia ya michango, historia ya pensheni,
kufuatilia mafao, kujisajili katika Mfuko na pia PSPF ilikuwa ikitoa
vitambulisho vipya kwa wanachama wake.
Katika
kunogesha siku ya PSPF, Mfuko uliwaalika,
Balozi wa PSPF Mjomba Mrisho Mpoto, waigizaji wote wa kikundi cha Original
Komedi na Mboni Masimba mtangazaji na mwaandaaji wa kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa na kituo
cha Televisheni cha TBC, kwa udhamini wa PSPF.
Baadhi
ya wageni mashuhuri waliotembelea banda la PSPF wakati wa maonesho hayo ni
pamoja na Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Gaudentia Kabaka, Waziri wa
Kazi na Ajira, Mheshimiwa Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Shaaban
Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wengi.
Kwa
mwaka wa pili mfululizo Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukitenga siku maalum
wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (sabasaba) kwa
ajili ya kutoa elimu juu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na huduma zinazotolewa na
PSPF.
Msanii mahiri wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akiwa ameambatana na baadhi ya wasanii wa kundi la Original Komedi walipokuwa wakikatiza viunga vya saba saba.
Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Original Komedi wakionesha mbwembwe zao
Baadhi ya wadau wakiendelea kujiunga na mfuko huo wa PSPF ndani ya viunga vya saba saba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...