Mwanariadha wa Polisi Tanzania Fabian Nelson (kushoto) akishangilia na wanariadha wenzake kutoka Zimbabwer baada ya kuvalishwa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio za kilomita 10000 katika uwanja wa Mavuso nchini Swaziland wakati wa Michezo ya majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.nafasi ya kwanza na ya tatu ilikwenda kwa wanariadha kutoka Jeshi la Polisi la Zimbabwe(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Swaziland).
Mwanariadha wa Polisi Tanzania Fabian Nelson (wa pili) akipambana na wanariadha wengine katika mbio za kilomita 10000 katika uwanja wa Mavuso nchini Swaziland wakati wa Michezo ya majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika(SARPCCO) yanayoendelea nchini Swaziland.Fabian Nelson alishinda medali ya Fedha baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio hizo.
Hongera Fabian kwa ushindi huu unaoleta matarajio kwa matokeo mazuri zaidi siku zijazo.
ReplyDeleteHongera Fabian lakini pia hongereni sana NMB Bank kwa udhamini wenu...nimeiona alama yenu kwenye Jersey ya Fabian,natumai mtaendelea kujitoa kwenye michezo mbadala.
ReplyDeleteHongera Nelson Fabia kwa medali yako ya fedha.
ReplyDeleteMwandishi ilikuwa ni mita 10,000.
Sio KILOMITA 10,000.