Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Clara Mwatuka, amefariki dunia jioni ya leo kwa ajali baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuelekea Ndanda, Masasi, mkoani Mtwara.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake,ambaye inasemekana ni mwanae. Maiti  ya marehemu imehifadhiwa katika  Hospitali ya Rufaa ya Ndanda.
Globu ya Jamii inaungana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu, na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi
Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...