Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Clara Mwatuka, amefariki dunia jioni ya leo kwa ajali baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuelekea Ndanda, Masasi, mkoani Mtwara.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake,ambaye inasemekana ni mwanae. Maiti ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda.
Globu ya Jamii inaungana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu, na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi
Amina.
Rip mh Mwatuka
ReplyDelete