Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni  kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Wajumbe

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-
1.
KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
1. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mwenyekiti
2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara
3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar
4. Ndugu Sofia Simba
5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
6. Ndugu Asha-Rose Migiro
7. Ndugu Samwel Sitta
8. Ndugu Nape Nnauye
9. Ndugu Mwigulu Nchemba
10. Ndugu Harrison Mwakyembe
11. Ndugu January Makamba
12. Ndugu Amina Makillagi
13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
14. Ndugu Stephen Wasira
15. Ndugu Abdallah Bulembo
16. Ndugu Hadija Aboud
17. Ndugu Mohamed Aboud
18. Ndugu Lazaro Nyalandu
19. Ndugu Issa Haji Ussi
20. Ndugu Waride Bakari Jabu
21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23. Ndugu Maua Daftari
24. Ndugu Stephen Masele
25. Ndugu Pindi Chana
26. Ndugu Shaka Shaka
27. Ndugu Makongoro Nyerere
28. Ndugu Bernard Membe
29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
30. Ndugu Antony Diallo
31. Ndugu Livingston Lusinde
32 . Ndugu Ummy Mwalimu


Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI

18/08/2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kampeni za uchaguzi wa Oktoba zitakapoanza zionyeshe ukomavu wa kisiasa wa vyama vyote vitakavyoshiki na wakereketwa wao.

    Vijana waelewe kuwa amani ya nchi hii ni muhimu, vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyotokana na jazba za kisiasa havikubaliki. Vyama na Wagombea wawaelekeze mashabiki wao waelekeze kampeni katika sehemu zilizopangwa ili polisi wasilazimike kutumia nguvu kama siku za hivi karibuni. Wakereketwa wa kampeni wasisababishe kufunga barabara, kuvamia maofisi, au sehemu za umma kwa makelele, wala kuwazuia wasiojihusisha na siasa kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku za kujitafutia riziki. Kampeni ziwe za amani, zisizo na rushwa,chuki,bali zenye malumbano ya hoja za msingi zinazowezekana kufuatana na uwezo wa nchi hii siyo kudanganya wananchi kwa yasiyowezekana kwa sababu ya uhalisia wa uwezo mdogo wa kiuchumi. Kama nchi zilizoendelea malumbano ya kisiasa ya msimu wa uchaguzi yatuache kuwa nchi moja ya watanzania.

    ReplyDelete
  2. Ni kupiga kura na ushindi wa chama chetu ndiyo tunategemea mwezi wa kumi.

    ReplyDelete
  3. kumekucha mafuriko yanakauka- NASUBIRI UKAWA wahame nchi

    ReplyDelete
  4. MIE WASIWASI WANGU POLISI TU WANAWEZA KUHARIBU KILA KITU.....

    ReplyDelete
  5. Eti Kibajaji naye yumo, hivi Kibajaji huwa wanampendea matusi yake?

    ReplyDelete
  6. Mmenifurahisha sana kumuweka Bw. Livingstone Lusinde (Kibajaji) kwenye hizi kampeni kwani yeye kupenda kuwaambia ukweli upande wa pili bila kumung'unya maneno! Big up CCM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...