Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi,katika
Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam
kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu
Oktoba 2015,ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Wajumbe
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa
jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika
katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam
chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha
kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida
Mashariki na Kiteto.
Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).
Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-
1.
KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
1. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mwenyekiti
2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara
3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar
4. Ndugu Sofia Simba
5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
6. Ndugu Asha-Rose Migiro
7. Ndugu Samwel Sitta
8. Ndugu Nape Nnauye
9. Ndugu Mwigulu Nchemba
10. Ndugu Harrison Mwakyembe
11. Ndugu January Makamba
12. Ndugu Amina Makillagi
13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
14. Ndugu Stephen Wasira
15. Ndugu Abdallah Bulembo
16. Ndugu Hadija Aboud
17. Ndugu Mohamed Aboud
18. Ndugu Lazaro Nyalandu
19. Ndugu Issa Haji Ussi
20. Ndugu Waride Bakari Jabu
21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23. Ndugu Maua Daftari
24. Ndugu Stephen Masele
25. Ndugu Pindi Chana
26. Ndugu Shaka Shaka
27. Ndugu Makongoro Nyerere
28. Ndugu Bernard Membe
29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
30. Ndugu Antony Diallo
31. Ndugu Livingston Lusinde
32 . Ndugu Ummy Mwalimu
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
18/08/2015
2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara
3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar
4. Ndugu Sofia Simba
5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
6. Ndugu Asha-Rose Migiro
7. Ndugu Samwel Sitta
8. Ndugu Nape Nnauye
9. Ndugu Mwigulu Nchemba
10. Ndugu Harrison Mwakyembe
11. Ndugu January Makamba
12. Ndugu Amina Makillagi
13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
14. Ndugu Stephen Wasira
15. Ndugu Abdallah Bulembo
16. Ndugu Hadija Aboud
17. Ndugu Mohamed Aboud
18. Ndugu Lazaro Nyalandu
19. Ndugu Issa Haji Ussi
20. Ndugu Waride Bakari Jabu
21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23. Ndugu Maua Daftari
24. Ndugu Stephen Masele
25. Ndugu Pindi Chana
26. Ndugu Shaka Shaka
27. Ndugu Makongoro Nyerere
28. Ndugu Bernard Membe
29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
30. Ndugu Antony Diallo
31. Ndugu Livingston Lusinde
32 . Ndugu Ummy Mwalimu
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
18/08/2015
Kampeni za uchaguzi wa Oktoba zitakapoanza zionyeshe ukomavu wa kisiasa wa vyama vyote vitakavyoshiki na wakereketwa wao.
ReplyDeleteVijana waelewe kuwa amani ya nchi hii ni muhimu, vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyotokana na jazba za kisiasa havikubaliki. Vyama na Wagombea wawaelekeze mashabiki wao waelekeze kampeni katika sehemu zilizopangwa ili polisi wasilazimike kutumia nguvu kama siku za hivi karibuni. Wakereketwa wa kampeni wasisababishe kufunga barabara, kuvamia maofisi, au sehemu za umma kwa makelele, wala kuwazuia wasiojihusisha na siasa kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku za kujitafutia riziki. Kampeni ziwe za amani, zisizo na rushwa,chuki,bali zenye malumbano ya hoja za msingi zinazowezekana kufuatana na uwezo wa nchi hii siyo kudanganya wananchi kwa yasiyowezekana kwa sababu ya uhalisia wa uwezo mdogo wa kiuchumi. Kama nchi zilizoendelea malumbano ya kisiasa ya msimu wa uchaguzi yatuache kuwa nchi moja ya watanzania.
Ni kupiga kura na ushindi wa chama chetu ndiyo tunategemea mwezi wa kumi.
ReplyDeletekumekucha mafuriko yanakauka- NASUBIRI UKAWA wahame nchi
ReplyDeleteMIE WASIWASI WANGU POLISI TU WANAWEZA KUHARIBU KILA KITU.....
ReplyDeleteNgoma ngumu sana!
ReplyDeleteEti Kibajaji naye yumo, hivi Kibajaji huwa wanampendea matusi yake?
ReplyDeleteMmenifurahisha sana kumuweka Bw. Livingstone Lusinde (Kibajaji) kwenye hizi kampeni kwani yeye kupenda kuwaambia ukweli upande wa pili bila kumung'unya maneno! Big up CCM
ReplyDelete