Deo Filikunjombe (CCM)
Na matukiodaimaBlog Ludewa
ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew Mkinga kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri alisema jana kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo kumkabidhi barua rasmi Filikunjombe ya kupita bila kupingwa
Waziri alisema kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa Wagombea wa DP na TLP walishindwa kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea huyo wa Chadema aliyereja fomu ya wadhamini bila kujaza tarehe ,mwezi wala mwaka ambao uchaguzi mkuu utafanyika .
Lugha gongana au udaku umeshaanza, unaposema amepita bila kupingwa hali ya kua kulikua na washindani wengine tena ambao hawakushiriki uchaguzi hueleweki.Vilevile hueleweki unaposema washindani wenzake wameingia mitini hali ya kua ukweli ni kwa hawakutimiza mashariti ya ugombea.Kwakweli ni msiba mkubwa ktk fani ya uandishi.
ReplyDeleteSijui huo ni utaratibu gani wa ki demokrasia. Ni vizuri kila mtu apigiwe kura hata kama ni peke yake. Kuwe na kura ya ndiyo au hapana. Za hapana zikizidi basi huyo wananchi hawamtaki. Na zoezi lianaze upya la kuchangua mwingine. Hapana shaka Bwana Filikunjombe atakuwa Mbunge mzuri lakini utaratibu huu wa kupitishwa bila kupingwa una walakini. serikaliipitie tena sheria hizi.
ReplyDelete