Deo  Filikunjombe (CCM)

Na  matukiodaimaBlog Ludewa 
ALIYEKUWA  mbunge   wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  amepita  bila kupingwa  baada ya  mgombea  wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew Mkinga  kushindwa  kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw  Wiliam Waziri alisema  jana   kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo  kumkabidhi  barua  rasmi Filikunjombe   ya kupita  bila  kupingwa
Waziri alisema   kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;

Kuwa Wagombea wa DP na TLP walishindwa  kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi. 

Mgombea   huyo  wa Chadema  aliyereja  fomu  ya  wadhamini  bila  kujaza tarehe  ,mwezi  wala mwaka ambao uchaguzi  mkuu utafanyika .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Lugha gongana au udaku umeshaanza, unaposema amepita bila kupingwa hali ya kua kulikua na washindani wengine tena ambao hawakushiriki uchaguzi hueleweki.Vilevile hueleweki unaposema washindani wenzake wameingia mitini hali ya kua ukweli ni kwa hawakutimiza mashariti ya ugombea.Kwakweli ni msiba mkubwa ktk fani ya uandishi.

    ReplyDelete
  2. Sijui huo ni utaratibu gani wa ki demokrasia. Ni vizuri kila mtu apigiwe kura hata kama ni peke yake. Kuwe na kura ya ndiyo au hapana. Za hapana zikizidi basi huyo wananchi hawamtaki. Na zoezi lianaze upya la kuchangua mwingine. Hapana shaka Bwana Filikunjombe atakuwa Mbunge mzuri lakini utaratibu huu wa kupitishwa bila kupingwa una walakini. serikaliipitie tena sheria hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...