Mzee Paul Sozigwa (pichani) ambaye alipotea tangu Jumapili mchana katika mazingira ya kitatanishi amepatikana akiwa salama salimini.
Kwa mujibu wa ujumbe kutoka kwa familia Mzee Sozigwa, alipatikana jana (Jumatatu) usiku na kwamba hali yake ni njema.  Mzee Sozigwa aliwahi  kuwa Mwandishi wa Habari  wa Rais katika serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Nyerere. 
"Asante sana kaka Michuzi. Tunaamini ya kwamba kutokana na tangazo kwenye blog yako imefanikisha zoezi zima na Baba amepatikana jana usiku. Mungu Akubariki sana!" ilisema taarifa hiyo iliyoletwa Globu ya Jamii leo na Salome Sozigwa Mjema

Taarifa ya awali ya familia, mara ya mwisho Mzee Sozigwa alionekana kanisani Mbezi Beach BCIC (kwa Gamanywa) jijini Dar es salaam Jumapili iliyopita saa nane mchana. Kupotea huko kulileta mashaka hasa kwa kuwa Mzee Sozigwa ni mgonjwa wa Alzheimer, na mara nyingi huwa anapoteza kumbukumbu. 

Globu ya Jamii inapenda kuipongeza familia ya Mzee Sozigwa na kuishukuru kwa kuonesha imani yake kwetu wakati wa changamoto hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Yahya SamejaAugust 11, 2015

    Way to go Ankal
    Above all it is the most read blog in earth in our native language.
    Ahsante Ankal

    ReplyDelete
  2. Glad to hear he has been found, salama usalimin.
    I was following the news for I know this young man. We were together Tabora school and later Makerere
    God bless,thanks Michuzi blog
    Wakatabahu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...