MNAMO TAREHE
14.08.2015 MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA ALIKUJA MKOA WA MBEYA AKIWA
AMEANDAMANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA CUF, NCCR – Mageuzi NA NLD KWA DHUMUNI LA
KUMTAMBULISHA NA KUOMBA UDHAMINI WA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA KWA NAFASI
YA URAIS.
KATIKA MSAFARA WAKE
KUTOKA UWANJA WA NDEGE [SONGWE] KULIONEKANA GARI MOJA (PICHANI) AINA YA LAND CRUISER –
PICK UP YENYE RANGI NYEUSI NA NDANI YAKE LILIKUWA LIMEBEBA VIJANA AMBAO
WALIKUWA WAMEVAA MAVAZI MEUSI, KOFIA – BERETI NYEUSI NA MIWANI NYEUSI NA MABUTI.
WATU HAO WALIKUWA NA MUONEKANO KAMA ASKARI NA SHUGHULI WALIYOKUWA WAKIFANYA YA KUONGOZA
MSAFARA, ULINZI NA KAZI NYINGINE ZIFANYAZO NA JESHI LA POLISI.
KUTOKANA NA MUONEKANO
WAO NA SHUGHULI WALIZOKUWA WAKIZIFANYA ILIKUWA IKITAFSIRIKA KUWA NI JESHI LIFANYAZO
KAZI HIZO AMBALO HALIKUWA LIKIFAHAMIKA.
KUTOKANA NA SINTOFAHAMU
HIYO WANANCHI WENGI WALIKUWA WAKIHOJI “HILO NI JESHI GANI” SAMBAMBA NA KUTUMA
PICHA KWA NJIA YA MTANDAO WA KIJAMII [WHATSAPP] WAKIONYESHA WASIWASI WALIOKUWA
NAO DHIDI YA KIKUNDI HICHO.
KUFUATIA HALI HIYO,
OFISI YA MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MBEYA ILIFUNGUA JALADA LA
UCHUNGUZI ILI KUWAPATA VIJANA WALE KWA LENGO LA KUWAHOJI NA KUKAMILISHA
UPELELEZI ILI JALADA LIPELEKWE KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA UFAFANUZI WA
KISHERIA. HII NI KUTOKANA NA KUIBUKA KWA MAKUNDI YA AINA HII HASA KWA VYAMA
VIKUBWA VYA SIASA HAPA NCHINI.
KATIKA KUFANYA
UFUATILIAJI HUO, WAPO WATU WAWILI WALIKAMATWA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 18.08.2015 KWA MAHOJIANO NA
BAADA YA MAELEZO YAO KUCHUKULIWA WALIPEWA DHAMANA.
BAADHI YA VIONGOZI WAO
WALIOKUJA POLISI WAMEELEZWA KUHITAJIKA KWA VIJANA WALE WALIOKUWA KATIKA GARI
LILE ILI WAHOJIWE NA KUKAMILISHA UPELELEZI WA JALADA HILO MAPEMA ILI
MWANASHERIA WA SERIKALI ALITOLEE MWONGOZO WA KISHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA.
sioni tatizo lolote ili mradi hawajashika silaha au kuingilia kazi za polisi. ni mbwembwe tu - MSIWE NA WIVU. mbona hamuulizii misafara ya boda boda kwenye kampeni?
ReplyDeleteHivi vyama vya upinzani wakiwa na chipukizi wao mtawakataza?
ni bora bubadili mtazamo hasi wa chama kimoja kwa maana kila kitu kinachokubalika lazima kifanywe na CCM au dola tu.
mnapoteza resource na muda kufuatilia mambo yasiyo na tija (sababu hapa hakuna suala lolote la kisheria). cha ajabu na huyo mwanasheria mkuu atatoa jibu haraka wakati kuna mambo mengi ya kisheria hayajashughulikiwa muda mrefu na waathirika wanaozea mahabusu -hasa kesi za mauaji!
Polisi wetu wamekuwa watu wa hovyo kabisa. Ni wavivu wa kufikiri na hata kujenga hoja.
ReplyDeleteHIvi Mbona hamtishiwi na wale vijana wa UVCCM na yale mavazi yao na mbwembwe zao za kikomandoo? Na badala yake mnakomaa na hawa wa upinzani tu tu?
Basi kama ni hivyo kamateni basi na wale Mabodigadi wa Viongozi wote wa upinzani maana nao wameanza kuwa mbwembwe za kuvaa suti na tai, miwani mweusi na vidude vya masikioni huku wakining'ia kwenye MA VX kama wale wa ikulu! Maana mmekuwa watu wa kukurupuka bila kujenga hoja makini Wananchi tumemichoka sasa.
Na wewe Michuzi wacha (kutumika) kutubania na kuwa bias kwa sisi watoa hoja.
Nyie wadau hapo juu vipi? Nchi hii inaongozwa na sheria. Haiwezekani kila anayetaka kwenda Ikulu awe na kukundi chake cha Ntarahamwe na Mayi mayi au wanamgambo wake.
ReplyDeleteTujufunze yaliyowakuta majirani zetu. Mifano iko mingi na wala siyo ya mbali.
Acheno ushabiki usiokuwa na Tija. Vikinuka mtakuwa wa kwanza kukimbia. Tanzania inahitaji amani na utulivu ili iendelee.
Msumeno hukata mbele na nyumba, sheria ifuate mkondo wake, hivi vikosi vya vyama vinavyofanya kazi ya dola vidhibitiwe mapema kabla havijaleta madhara.
ReplyDeleteKweli jeshi la Polisi wa Tanzania halina maana ni mambo gani haya ya kufuatilia, Yale meno ya tembo yaliyokamatwa uswis mmeshindwa kufuatilia na kutupa jibu ilikuaje yakapita uwanja wa JK mnaangaika na watu waliovaa nguo zisizo hata za kwenu. Mnaelewa maana ya Uhuru nini? Kama wameamua kuvaa hata manyoya kama Askari wa jadi achaneni nao kwani si yao au ni wivu kwa vile walioneka wakakamavu kuwashindaa ninyi
ReplyDeleteendeleeni kuwapendelea tu hao ccm.
ReplyDeleteKulea vikundi vya usalama visivyo tambuliwa kisheria ndiko lkunakosababisha vikundi vya ugaidi kama Boko Haramu, na ISIS kama ilivyokwishaelezwa na msajili wa vyama kuruhusu hivi vikundi vikundi ni makosa, kama ni ulinzi walindwe na polisi inayotakiwa kutoa utumishi kwa wote.
ReplyDeleteHivi mimi nikilipa watu wavae hivi na kusindikiza gari langu mbele na nyuma bila kushika silaha nitakuwa nimevunja sheria? Mnataka mbwembwe zifanywe na watawala tu hakuna hoja ya kisheria hapa.
ReplyDeleteNa hasa wakat huu wa uchaguzi, polisi wanatumia ukandamizaji wa opposition (suppression) kama njia ya kuonekana loyal kwenye system na kupanda vyeo! Hili linafahamika.
ReplyDeletehi inaongozwa kwa mjibu wa sheria vyama husika lazima wategemee police siyo kama hivyo nahata watu wenyewe wanaonekana ni watu wa shari hivo serikali kuweni makini na w..tuuvikunachagadi
ReplyDeleteKamateni hata Kk, ultimate security
ReplyDeleteNa wale makamanda wanaovaa nguo za kijani na wanaopiga watu mbona hatuoni wakihojiwa? Polisi wetu wanafanya kazi kwa kujipendekeza hovyo kwa CCM, Kwanza mmeandika taarifa hii kwa hati kubwa mnamaanisha nini? Kwani kuvaa mabuti na combat kuna tatizo gani?
ReplyDeleteHawa polisi inaelekea hawana cha kufanya au wanataka kutuonyesha kuwa wanafanya kazi. Hili siyo suala la kujadili. Hamna kosa lolote lililotenda na hao jamaa. Acheni kutumika, mtapata machungu siku wapinzani wakiingia madarakani.
ReplyDelete