MNAMO TAREHE 14.08.2015 MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA ALIKUJA MKOA WA MBEYA AKIWA AMEANDAMANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA CUF, NCCR – Mageuzi NA NLD KWA DHUMUNI LA KUMTAMBULISHA NA KUOMBA UDHAMINI WA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA KWA NAFASI YA URAIS.

KATIKA MSAFARA WAKE KUTOKA UWANJA WA NDEGE [SONGWE] KULIONEKANA GARI MOJA (PICHANI) AINA YA LAND CRUISER – PICK UP YENYE RANGI NYEUSI NA NDANI YAKE LILIKUWA LIMEBEBA VIJANA AMBAO WALIKUWA WAMEVAA MAVAZI MEUSI, KOFIA – BERETI NYEUSI NA MIWANI NYEUSI NA MABUTI. WATU HAO WALIKUWA NA MUONEKANO KAMA ASKARI NA SHUGHULI WALIYOKUWA WAKIFANYA YA KUONGOZA MSAFARA, ULINZI NA KAZI NYINGINE ZIFANYAZO NA JESHI LA POLISI.
  
KUTOKANA NA MUONEKANO WAO NA SHUGHULI WALIZOKUWA WAKIZIFANYA ILIKUWA IKITAFSIRIKA KUWA NI JESHI LIFANYAZO KAZI HIZO AMBALO HALIKUWA LIKIFAHAMIKA.
KUTOKANA NA SINTOFAHAMU HIYO WANANCHI WENGI WALIKUWA WAKIHOJI “HILO NI JESHI GANI” SAMBAMBA NA KUTUMA PICHA KWA NJIA YA MTANDAO WA KIJAMII [WHATSAPP] WAKIONYESHA WASIWASI WALIOKUWA NAO DHIDI YA KIKUNDI HICHO.
KUFUATIA HALI HIYO, OFISI YA MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MBEYA ILIFUNGUA JALADA LA UCHUNGUZI ILI KUWAPATA VIJANA WALE KWA LENGO LA KUWAHOJI NA KUKAMILISHA UPELELEZI ILI JALADA LIPELEKWE KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA UFAFANUZI WA KISHERIA. HII NI KUTOKANA NA KUIBUKA KWA MAKUNDI YA AINA HII HASA KWA VYAMA VIKUBWA VYA SIASA HAPA NCHINI.
KATIKA KUFANYA UFUATILIAJI HUO, WAPO WATU WAWILI WALIKAMATWA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 18.08.2015 KWA MAHOJIANO NA BAADA YA MAELEZO YAO KUCHUKULIWA WALIPEWA DHAMANA. 
BAADHI YA VIONGOZI WAO WALIOKUJA POLISI WAMEELEZWA KUHITAJIKA KWA VIJANA WALE WALIOKUWA KATIKA GARI LILE ILI WAHOJIWE NA KUKAMILISHA UPELELEZI WA JALADA HILO MAPEMA ILI MWANASHERIA WA SERIKALI ALITOLEE MWONGOZO WA KISHERIA.
  
           Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sioni tatizo lolote ili mradi hawajashika silaha au kuingilia kazi za polisi. ni mbwembwe tu - MSIWE NA WIVU. mbona hamuulizii misafara ya boda boda kwenye kampeni?
    Hivi vyama vya upinzani wakiwa na chipukizi wao mtawakataza?
    ni bora bubadili mtazamo hasi wa chama kimoja kwa maana kila kitu kinachokubalika lazima kifanywe na CCM au dola tu.

    mnapoteza resource na muda kufuatilia mambo yasiyo na tija (sababu hapa hakuna suala lolote la kisheria). cha ajabu na huyo mwanasheria mkuu atatoa jibu haraka wakati kuna mambo mengi ya kisheria hayajashughulikiwa muda mrefu na waathirika wanaozea mahabusu -hasa kesi za mauaji!

    ReplyDelete
  2. Polisi wetu wamekuwa watu wa hovyo kabisa. Ni wavivu wa kufikiri na hata kujenga hoja.

    HIvi Mbona hamtishiwi na wale vijana wa UVCCM na yale mavazi yao na mbwembwe zao za kikomandoo? Na badala yake mnakomaa na hawa wa upinzani tu tu?

    Basi kama ni hivyo kamateni basi na wale Mabodigadi wa Viongozi wote wa upinzani maana nao wameanza kuwa mbwembwe za kuvaa suti na tai, miwani mweusi na vidude vya masikioni huku wakining'ia kwenye MA VX kama wale wa ikulu! Maana mmekuwa watu wa kukurupuka bila kujenga hoja makini Wananchi tumemichoka sasa.

    Na wewe Michuzi wacha (kutumika) kutubania na kuwa bias kwa sisi watoa hoja.

    ReplyDelete
  3. Nyie wadau hapo juu vipi? Nchi hii inaongozwa na sheria. Haiwezekani kila anayetaka kwenda Ikulu awe na kukundi chake cha Ntarahamwe na Mayi mayi au wanamgambo wake.

    Tujufunze yaliyowakuta majirani zetu. Mifano iko mingi na wala siyo ya mbali.

    Acheno ushabiki usiokuwa na Tija. Vikinuka mtakuwa wa kwanza kukimbia. Tanzania inahitaji amani na utulivu ili iendelee.

    ReplyDelete
  4. Msumeno hukata mbele na nyumba, sheria ifuate mkondo wake, hivi vikosi vya vyama vinavyofanya kazi ya dola vidhibitiwe mapema kabla havijaleta madhara.

    ReplyDelete
  5. Kweli jeshi la Polisi wa Tanzania halina maana ni mambo gani haya ya kufuatilia, Yale meno ya tembo yaliyokamatwa uswis mmeshindwa kufuatilia na kutupa jibu ilikuaje yakapita uwanja wa JK mnaangaika na watu waliovaa nguo zisizo hata za kwenu. Mnaelewa maana ya Uhuru nini? Kama wameamua kuvaa hata manyoya kama Askari wa jadi achaneni nao kwani si yao au ni wivu kwa vile walioneka wakakamavu kuwashindaa ninyi

    ReplyDelete
  6. endeleeni kuwapendelea tu hao ccm.

    ReplyDelete
  7. Kulea vikundi vya usalama visivyo tambuliwa kisheria ndiko lkunakosababisha vikundi vya ugaidi kama Boko Haramu, na ISIS kama ilivyokwishaelezwa na msajili wa vyama kuruhusu hivi vikundi vikundi ni makosa, kama ni ulinzi walindwe na polisi inayotakiwa kutoa utumishi kwa wote.

    ReplyDelete
  8. Hivi mimi nikilipa watu wavae hivi na kusindikiza gari langu mbele na nyuma bila kushika silaha nitakuwa nimevunja sheria? Mnataka mbwembwe zifanywe na watawala tu hakuna hoja ya kisheria hapa.

    ReplyDelete
  9. Na hasa wakat huu wa uchaguzi, polisi wanatumia ukandamizaji wa opposition (suppression) kama njia ya kuonekana loyal kwenye system na kupanda vyeo! Hili linafahamika.

    ReplyDelete
  10. hi inaongozwa kwa mjibu wa sheria vyama husika lazima wategemee police siyo kama hivyo nahata watu wenyewe wanaonekana ni watu wa shari hivo serikali kuweni makini na w..tuuvikunachagadi

    ReplyDelete
  11. Kamateni hata Kk, ultimate security

    ReplyDelete
  12. Na wale makamanda wanaovaa nguo za kijani na wanaopiga watu mbona hatuoni wakihojiwa? Polisi wetu wanafanya kazi kwa kujipendekeza hovyo kwa CCM, Kwanza mmeandika taarifa hii kwa hati kubwa mnamaanisha nini? Kwani kuvaa mabuti na combat kuna tatizo gani?

    ReplyDelete
  13. Hawa polisi inaelekea hawana cha kufanya au wanataka kutuonyesha kuwa wanafanya kazi. Hili siyo suala la kujadili. Hamna kosa lolote lililotenda na hao jamaa. Acheni kutumika, mtapata machungu siku wapinzani wakiingia madarakani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...