Mwandishi wa makala haya Bw. Yusuph Kileo akitoa mada kwenye moja ya vikao vya usalama mitandao jijini Nairobi, Kenya, hivi karibuni |
Nimekamilisha vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini
Nairobi kufuatia mualiko maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha
mada mbili (ya kwanza ikiwa ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada
ya pili ikiwa ni namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada
hizo mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna
mengi nikajifunza kutoka kwa washiriki.
Aidha, nilishiriki mijadala duara
iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu mitandao na kuiangazia
sharia mtandao ya nchi ya Kenya.
Kenya ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo
zimeorodheshwa kuwa na uhalifu mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria
pamoja na Afrika ya kusini.
Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote,
tulishuka na kuangazia bara la Afrika na baadae Afrika mashariki na hatimae
kujikita na takwimu za nchi ya Kenya.
Kwa upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizo wasilishwa katika
mkutano, hadi kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8
Milioni huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha, matumizi ya
intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”. Takwimu hizo
zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil) kila mwaka
kutokana na uhalifu mtandao.
Ndugu Kileo,
ReplyDeleteHongera kwa kutuwakilisha, na shukrani kwa taarifa. Huwa napenda kujifunza mambo mapya, na kwa msingi huo umenipa changamoto. Nakutakia kila la heri.