Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino
(kulia) akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita - Manzie
Mangochie (kushoto) kwa niaba ya Shule za Msingi Nyamkumbu na Ukombozi
msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi
milioni 10 kutoka Benki ya NMB katika hafla fupi iliyofanyika mjini
Geita jana ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
Wanafunzi wa Shule za Msingi Nyankumbu wakiwa na
nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 na Benki ya
NMB jana wilayani Geita.NMB ilisaidia madawati 100 yenye thamani ya
Shilingi milioni 10 katika shule mbili za msingi
za Nyamkumbu na Ukombozi ambapo kila shule ilipata madawati 50
BENKI ya NMB jana ilikabidhi msaada wa madawati 100
yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shule za Msingi Nyankumbu na
Ukombozi zilizopo mkoani Geita ambapo kila shule imekabidhiwa madawati
50.
Msaada huo umekabidhiwa na meneja wa NMB Kanda ya
Ziwa - Abraham Augustino ambapo mkuu wa wilaya ya geita alipokea
madawati hayo kwa niaba ya shule hizo mbili za msingi.
“Madawati haya tunayoyakabidhi leo ni moja ya
ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza
Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida
tunayoipata,” alisema Augustino.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...