Mratibu wa Mradi wa kuzalisha gesi ambaye pia ni
mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika fani ya Uhandisi wa Mazingira, Chuo
Kikuu cha Ardhi John Rutahirwa Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu moja ya mtambo wa kukusanyia maji taka kutoka majumbani eneo
la mradi wa kuzalisha gesi Vingunguti.Gesi hiyo itaanza kutumika mwezi
Desemba mwaka huu.
Jumanne Saidi Fundi ujenzi wa vyoo na msimamizi wa mradi wa
majaribio wa Biogasi Vingunguti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu kazi ya ufungaji wa miundombinu ya kuzalisha gesi katika eneo la
Vingunguti.
Mtambo wa kuzalisha Gesi katika katika eneo la Mradi wa
Majaribio eneo la Vingunguti unaokusanya maji taka moja kwa moja kutoka
katika makazi ya wananchi.Mtambo huo kwa mujibu wa maelezo ya watalaam
wa mradi huo una uwezo wa kukaa ardhini kwa kipindi cha miaka 50.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...