HOSPITALI ya Taifa Muhimbili –MNH- imetoa mafunzo kwa watumishi wake kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ambao umesambaa
na kusababisha watu 989 kuambukizwa ugonjwa huo jijini
Dar es salaam.
Mafunzo hayo ya siku saba ambayo
yanahusisha Wakurugenzi, Wakuu wa Idara , Madaktari, Wauguzi , Wafamasia pamoja
na Wahudumu yana lengo la kuwaelimisha
juu ya ugonjwa huo , jinsi ya kuzuia , kumtibu mgonjwa na kumtambua mtu mwenye
dalili za Kipindupindu.
Akielezea mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya magonjwa ya
dharura na ajali ambaye pia ni
Daktari Bingwa wa magonjwa hayo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dokta
JUMA MFINANGA amesisitiza kuwa chanzo kikuu cha
ugonjwa wa Kipindupindu ni uchafu lakini pia maji machafu yanachangia kwa asilimia kubwa kuenea
kwa ugonjwa huo.
SIKU SABA KUFUNDISHWA JINSI YA KUZUIA KIPINDUPINDU, HUU NI UPUUZI MTUPU. KIPINDUPINDU NI UGONJWA WA UCHAFU. MTU AKILA MAVI NDO ANAUPATA, NA MAVI SIYO LAZIMA YAONEKANE, KWANI KWENYE MAJI MACHAFU, VYAKULA VICHAFU, MIKONO MICHAFU, VIPOLO VICHAFU, CHA MAANA NI USAFI BINAFSI NA MAZINGIRA. VIBRIO CHOLERAE ANAPENDA UCHAFU. HUITAJI SIKU SABA KUWAFUNDISHA WATU WAZIMA KUHUSU CHOLERA.
ReplyDelete