
Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720.
Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na
asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu
inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata
nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.
Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake.
Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake.
Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika
majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi
wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania
wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani
na sera za CCM.
Endeleza kampeni CCM ni kuwatakia tu ushindi wa kishindo.
ReplyDeleteHadi jana Tarehe 16. Leo ndo tarehe 16 kuna kosa la uandishi au?
ReplyDeleteKwa kuwa hiyo tathmini mmeifanya ninyi wenyewe mnaweza kuipamba kwa aina yoyote ile inayo wapendeza. Intellectuals na wataalamu wa polls huwa wanasikiliza zaidi independent pollster au institutions. Sasa kinacho wadhuru ninyi ni ukweli kwamba hampendi tabiri zilizo huru zifanyike. Sasa huna haja ya kutoa matokeo haya kwenye jamii. Ungetuma kwa wana CCM wenzio ili muendelee kujipa false hopes.
ReplyDeleteWananchi wanasikiliza polls za asasi zilizo huru, sio hizi ambazo unaleta hapa. No where on earth CCM will get over 50% of votes in next election. Kikwete on his second term hakufikisha hizo asilimia unazotaja kwenye assesment yako.
Jidanganye mwenyewe na wachache wenzio.
Tanzanians are determined, and ready to proves you wrong.
Hata tabiri zilizohuru zikiuliza watu elfu moja wakati tuko milioni arobaini hazina uwakilishi wa ukweli wala sayansi yoyote katika nchi hii ya watu wenye uelewa na ushabiki usiosimamia itikadi. Hukuna cha independent pollster wala nini.
ReplyDelete