Bendera ya Palestine itapepea nje ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, hii inafuatia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio ambalo linatoa fursa kwa nchi ambazo si mwanachama kamili wa Umoja huo kupeperusha bendera yake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ubao wa Matangazo ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, ukionyesha matokeo ya kura katika tukio la kihistoria
kufanyika ambapo Baraza hilo limepitisha azimio linalotoa fursa kwa
Palestina kupeperusha bendera yake. Nchi wanachama walipiga makofi
kushangilia kupitishwa kwa azimio hilo, ambalo Israel imesema Palestina
inatafuta umaarufu kwa njia za mkato badala ya kurejea kwenye meza ya
mazugumzo.
Na
Mwandishi Maalum New York
BARAZA
Kuu la Umoja wa Mataifa, jana Alhamis,
limepitisha Azimio ambalo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Umoja huo, litaruhusu
nchi ambazo siyo mwanachama kamili kupeperusha bendera yake katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kupitishwa
kwa azimio hilo ambalo limepigiwa
kura za ndiyo 119 za hapana nane
na zisizofungamana na upande wowote 45 kunaipa fursa Palestina kupeperusha bendera yake nje ya Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa.
Mara
baada ya matokeo ya kura kutangazwa
rasmi, Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipiga makofi kama ishara ya
kufurahia kupitishwa kura nyingi azimio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...