Na: Moh’d Said
Shule ya msingi ya mtemani Wingwi iliyoko Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, imekabidhiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya ujenzi na uanzishaji wa maktaba ya kisasa (Digital Library) inayaotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Tukio hilo lilifanyika leo katika viwanja vya shule ya mtemani mbele ya kamati ya shule hiyo ambapo muhisani na mdau wa maendeleo nchini ambaye pia ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha London, SOAS, Bwana Yussuf Shoka Hamad alikabidhi zawadi hizo kama sehemu ya ahadi zake alizozitoa mwaka jana katika hafla ya kuwazawadia wanafunzi waliofaulu vizuri darasa la saba mwaka 2013/14.
Akikabidhi zawadi hizo, Bwana Yussuf Shoka Hamad alisema; ‘Nia yangu ni kuleta mapinduzi ya kweli kwa jamii katika sekta ya elimu. Mapinduzi ya kweli kwa ulimwengu wa sasa yanatokana na kutegemea sana maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hivyo, katika kipindi hiki cha miaka mitano (2015/20) nimenuilia kuanzisha maktaba za kisasa (digital libraries) kwa shule zote za Wingwi ili kusukuma mbele maendeleo ya elimu’
Aidha mhisani huyo alisema kwamba wakati umefika kwa wanakijiji wa Wingwi kuamka na kuipa kipaumbele sekta ya Elimu kwa watoto wao kwani Elimu ndio silaha tosha inayoweza kuleta Mapinduzi nchini.
Pia aliwasisitiza wanakamati wa shule hiyo, kuthamini michango inayotolewa na wahisani na wazazi wa wanafunzi kwa kutunza na kuenzi kila msaada unaopatiwa shuleni hapo.
Mwalimu mkuu wa shule ya Mtemani Bi Wahida Saleh alisema, anashukuru sana kupokea vifaa hivyo na ameahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo ili kuweza kuleta matunda yanayotazamiwa kupatikana kutokana na uanzishwaji wa maktaba hiyo shuleni hapo.
Naye, mdau wa Elimu na mwanakamati wa shule hiyo Bwana Shoka Hamad Abeid ameinasihi kamati na jamii kwa ujumla kuvitunza vifaa hivyo na kuvienzi kwani kufanya hivyo kutepelekea lengo zima la kulete ufanisi shuleni hapo kufikiwa
Bwana
Yussuf Shoka Hamad akimkabidhi pazia la
projector kwa ajili ya maktaba ya shule hio Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mtemani, Wingwi Bi Wahida Saleh Hamad
katika hafla fupi ya kukabidhiana vifaa iliyofanyika shuleni hapo
Mwalimu
Mkuu, shule ya msingi Mtemani, Wingwi akipokea Mashine ya Kompyuta kwa ajili ya maktaba ya shule hio kutoka kwa
muhisani wao Bwana Yussuf Shoka Hamad
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...