MUIMBAJI nguli wa muziki
Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuwasha moto kwenye jukwaa la Tamasha la
Amani ambalo litarajia kufanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Msama Promotions, Alex Msama mwimbaji huyo ndiye atakayekoleza maombi ya amani
ya Tanzania ambayo inapigiwa chapuo la kulindwa kila kukicha.
Msama alisema hivi sasa Kamati
yake inaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo ni chachu ya
amani hasa kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 kwa nafasi za
urais, Ubunge na Udiwani.
Aidha Msama alisema Kamati yake
inaendelea na mawasiliano na waimbaji wa nchi za Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi
na Uingereza ambazo ni mojawapo ya nchi ambazo ni kichocheo cha amani ya Tanzania.
“Kwa kuwa tumejipanga kumpigia
magoti Mungu ili kuilinda amani yetu, hatuna budi kuwashirikisha pia wadau
mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali sambamba na waimbaji ambao watakaoimba nyimbo
ambazo zitachochea amani,” alisema Msama.
Msama alisema tamasha hilo
litahudhuriwa na viongozi wa kada ya siasa ambao watakuwa ndio walengwa ambao
wanatakiwa kutoa somo kwa vijana ambao wamejikita katika siasa bila ya kuwa na
weledi wa siasa.“Tutakuwa na matukio mengi
ambayo ni viashiria vya kuombea amani Tanzania ambako pia kutakuwa na tuzo
maalum ambazo watakabidhiwa baadhi ya viongozi ambao mchango wao katika jamii,”
alisema Msama.
Mwisho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...