Kuna mtu anatumia akaunti feki ya msanii wa Yamoto Band Enock Bella akiomba kutumiwa rambirambi ya msiba wa mama mzazi wa Aslay Isihaka Ambaye amefariki Dunia leo asubuhi.
Mtu huyo anatumia namba 0716281999 na amesajili kwa jina la Aslay Isihaka tunawaomba wadau na mashabiki wa Yamoto Band na Aslay wapuuze tariifa siyo za ukweli na hakuna utaratibu wa kutuma rambirambi katika simu.
Vijana wa aina hii ndiyo wa kukamatwa na hiyo sheria ya mtandao.
ReplyDeleteKwanini anamzulia mama wa mwenzake kufariki? Au ndiyo njia rahisi ya kupata fedha kama alivyoainisha kwenye namba yake.
AKAMATWE HARAKA ILI WENGINE WASIZOEE