Haya ndiyo Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (Ajenda 2030) ambayo leo Ijumaa Wakuu wa Nchi na Serikali wanayapitisha katika Mkutano wao wa Kihistoria Unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Ajenda 2030 ambayo utekelezaji wake unaaza mwakani inachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia( MDGs) ambayo yamefikia ukiongoni mwaka huu. Upitishaji wa Ajenda 2030 utatanguliwa na hotuba ya Baba Mtakatifu Francis
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani na Mashirika ya Kimataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani, Mkutano uliokuwa ukijadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uhusiano wake na usalama wa chakula, lishe na afya. Mkutano huu ulifanyika siku ya alhamis katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa
Sehemu ya washiri wa mkutano kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa usalama wa chakula, lishe na afya wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula ambaye alikuwa kati ya wanajopo watano waliozugumza katika mkutano huo.
Na Mwadishi Maalum,
New York
Leo Ijumaa,
Viongozi Wakuu wa Nchi na
Serikali zaidi ya 150 kutoka mataifa mbalimbali duniani, watapisha ajenda na malengo mapya ya
maendeleo endelevu ( Ajenda 2030) kuchukua
nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya
Millenia yanayomaliza muda wake mwishoni
mwa mwaka huu.
Katika mkutano huu wa
kihistoria unaofanyika miaka kumi na tano tangu MDGs zilizopitishwa,
utatanguliwa na hotuba ya Baba Mtakatifu Francis.
Baada ya
kupitisha ajenda 2030 na ambayo imejikita zaidi katika kuutokomeza umaskini na
ulinzi wa mazingira pasipo kumwacha yeyote nyuma,Viongozi hao Wakuu
wa Nchi na Serikali kila mmoja wao atapata fursa ya kuelezea matarajio ya serikali yake katika
utekelezaji wa ajenda hiyo yenye malengo 17.
Tayari Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wamekwisha kuwasili Jijini New York , yaliko
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku moja
kabla ya kupitishwa kwa ajenda
2030, baadhi ya viongozi ambao wameambatana na
Mhe. Rais wameshiriki katika mijadala mbalimbali na ambayo maudhui yake
yanashabihiana na ajenda nzima ya Maendeleo Endelevu.
Akiwakilisha ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo ya
pembezoni, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula, alishiriki katika majadiliano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na uendelevu wa usalama wa chakula, lishe na Afya
Balozi Mulamula
alikuwa kati ya wanajopo watano katika
majadiliano hayo ambayo yaliandaliwa na Wizara ya
Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo ya Ujerumani na
Mashirika ya Kimataifa .
Katika majadiliano hayo ambayo yalijikita katika
kuangalia ni namna gani utekelezaji
wa ajenda ya maendeleo endelevu unavyoweza kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hususani katika
maeneo yanayomgusa mwananchi wa kawaida kama vile usalama wa chakula, lishe na
afya.
Aidha wanajopo hao
walitakiwa kujibu hoja mbalimbali
zikiwamo ni kwa namna gani kwa mfano
Tanzania imejiandaa katika kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi na
ambayo kwayo kwa namna moja ama nyingine
yanaweza kuleta au yanasababisha matatizo katika eneo kama kilimo na lishe.
Akijibu hoja hiyo
pamoja na nyingine, Katibu Mkuu, Balozi
Liberata Mulamula aliwaeleza washiriki wa majadiliano hayo kwamba kwa nchi kama Tanzania mabadiliko ya tabia nchi ni jambo lililo dhahiri na si nadharia.
Akatoa mfano kwa
kusema kwamba, kuna baadhi ya maeneo ya nchi, ambapo wakulima wanashindwa kutambua msimu
halisi wa kuanza kulima na kupanda tofauti na miaka ya nyuma.
Aidha akasema, maeneo mengine mvua zinanyesha kupita kiasi
na wakati maeneo mengine yana kumbwa na
ukame wa kupindukia na hivyo kuathiri shughuli za kilimo na hatimaye ukosefu wa
chakula na chakula chenye viini
lishe ambavo ni muhimu kwa ukuaji na
maendeleo hususahi ya watoto chini
ya miaka mitano.
Mfano mwingine
ambao anasema ni wazi umechangia
kwa namna moja ama nyingine katika ubaribufu wa mazingira ni pamoja na
matumzi yasiyo endelevu ya ardhi,
ukataji wa holela wa miti
na ile hali ya mito mikubwa kupingukiwa maji na hivyo kufanya mabwana makubwa yanatuyotumika kuzalisha umeme kukosa maji ya
kutosha.
“Nilipokuwa mdogo
tulikuwa tunakatazwa sana na wazazi wetu kung’oa miti michanga, na wakati huo
hatukuelewa kwamba wazee wetu walikuwa wanatufundisha utunzaji wa miti” akasema
Balozi
Akielezea ni
mikakati gani ambayo serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali inachuka katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hiyo kuwa na uhakika wa usalama wa chakula,
na upatikanaji wa lishe bora.
Katibu Mkuu, ameeleza
kwamba serikali imejiwekea mipango madhubuti ikiwamo ya uhamasishaji wa wananchi kuwa na matumizi bora na endelevu ya ardhi,
misitu, kilimo cha umwagiliaji pasi
kutumia maji mengi na uhifadhi wa misitu.
Akasisitiza
kwamba mipango yote iwe
ile inayoandaliwa na Umoja wa Mataifa Mashirika ya Kimataifa n ahata
Serikali ili tekelezeka na kuwa endelevu
inapashwa kumilikiwa na wananchi ambao
hasa ndio waathirika wakubwa lakini pia
wanamchango mkubwa wa kuleta mabadiliko ili mradi wawezeshwe.
Akatahadharisha kwa
kusema kama wananchi hawatahusishwa kwa
namna moja ama nyingine basi
utekelezaji wa ajenda ya maendeleo
endelevu unaweza kuishia kwenye
makabrasha.
Wanajopo wengine
wakichangia katika majadiliano hayo
akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa Mapango wa
Chakula Duniani, walieleza kwamba suala na usalama wa chakula na lishe
linapashwa kupewa mkazo wa kipekee kwa kile walichosema, takwimu zinaonyea
kwamba idadi kubwa na watu duniani wanathirika kwa ukosefu wa chakula lakini
kubwa Zaidi vyakula vyenye virutubisho
na viini lishe.
Wakatoa mfano kwa kusema kuwa wakati bei ya vyakula aina ya nafaka ikushuka, bei ya matunda na mboga mboga, vyakula vitokanavyo na wanyama na ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa watoto
chini ya miaka mitano vinazidi kupanda bei maradufu na wanaoathirika ni watu maskini.
Na kwa sababu hiyo
wakasisitiza kwamba kuna uwiano mkubwa kati ya mabadiliko ya tabia nchi,
tatizo la usalama wa chakula na lishe duni mambo ambayo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zinatakiwa kushirikiana na kuikabili changamoto hii ambayo athari zake
ni kubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...