AIRTEL Tanzania yazindua kadi ya malipo ya 'Airtel Money Tap Tap'
• Airtel yawa kampuni ya kwanza kutoa huduma ya kufanya
malipo kwa kupitia kadi inayouunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya
mteja
Dar es Salaam, Jumatatu 12 Octoba 2015, Airtel Tanzania leo
imezindua huduma ya kwanza , ya kipekee na kibunifu yenye technologia
ya kisasa ijulikanayo kama “Tap Tap” itakayomuwezesha mtumiaji wa
huduma ya Airtel Money kufanya malipo kwa njia rahisi na,salama
kupitia kadi hiyo.
Huduma hii itawewazesha wateja na jamii kwa ujumla kutumia maendeleo
ya technologia kuleta urahisi katika kuendesha maisha yao. “Tap Tap”
itawawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala kwa haraka na
urahisi kwa kugusisha kadi zao ambazo zimeunganishwa na akaunti ya
Airtel money wakati wowote wanapotaka kulipia huduma mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel
Bi Jane Matinde alisema” Leo kwa mara nyingine tena Airtel tunachua
hatua thabiti katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wateja wetu
kupitia uzinduzi wa huduma hii ya Tap Tap.
Kadi hii ni rahisi
kutumia, ili kufanya malipo mteja atagusisha kadi yake kwenye kifaa
cha muuzaji na moja kwa moja kufanya malipo kwa kuweka namba yako ya
siri, wateja wetu wataweza kulipia huduma mbalimbali katika vituo vya
mafuta , maduka ya dawa, baa, saloni, maduka ya rejareja, wataweza
kununua muda wa maongezi kwa mawakala wa Airtel Money. Kupitia kadi
hii tunawawezesha watanzania kuwa na usalama na pesa zao na kuondoa
haja ya mteja kutembea na pesa wakati wote. vilevile Mteja
atakapopoteza au kuibiwa kadi hela zake zitakuwa bado ni salama”
Aliongeza kwa kusema , huduma ya “Tap Tap” inadhihirisha dhamira yetu
ya kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na
kutengeneza njia mpya ya kufanya malipo katika technologia ya simu za
mkononi na kuwaondolea wateja wetu athari zitakazowapata kwa kutembea
na pesa nyingi mfukoni
“ Tunaamini technologia hii mpya katika huduma za kifedha kupitia
simu za mkononi italeta njia mbadala wa kufanya malipo na pia kusaidia
katika kuendelea kukuza na kutanua huduma za kifedha nchini.”.
“Ni matumaini yetu kuwa wakazi katika maeneo ya Mbagala, Temeke,
Tandika, Ubungo ambapo huduma hii imezinduliwa kwaoleo watafurahia
faida zinazotokana na huduma hii ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi.
Jane Matinde akionyesha kadi mpya ya malipo inayotumia huduma ya Airtel
Money iliyopewa jina la Airtel Money ‘ Tap Tap’ katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa kadi hiyo uliofanyika mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama
hiyo ambapo mteja anaweza kuitumia kufanyia malipo mbalimbali hata kama
simu yake haipo hewani.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi.
Jane Matinde (wa pili kushoto) na Ofisa wa kitengo cha Airtel Money,
Stephen Kimea, wakiwapa baadhi ya wateja, Shabani Mneta (kulia) na
Penina Mneta, kadi za Airtel Money ‘Tap Tap’ mara baada ya
kuunganishwa katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa kadi hiyo ya malipo inayotumia huduma ya Aritel Money
katika kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza
ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...