Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa kutumia Vipodozi wakiwa kwenye mafunzo kwa njia ya Vitendo..Wanawake wachache wa jiji la Dar es salaam wameendelea kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Washiriki hawa wameendelea kufundishwa matumizi sahihi na ueledi wa kutumia vipodozi (makeup) mbalimbali kutokana na nyakati tofauti. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya urembo na muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo.
  Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa (paired) na Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii watakaowaita 'Mentor'. Mentor night kama dada wa kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. 
Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...