Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MSAJILI wa Vyama vya Siasa
nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi alisema kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25
kuweka kipaumbele cha amani ambayo isiweze kuharibiwa kwa kutokana na uchaguzi.
Mtungi aliyasema hayo alipokutana na
wahariri wa vyombo vya habari katika kusisitiza amani katika uchaguzi mkuu na
kutaka waandishi kutumia kalamu vizuri kwani amani ikiharibika hakuna anayebaki
salama.
Amesema matatizo ambayo yameanza
kutokea katika kamapeni yanayotokana na mtu mmoja yasiwekwe katika sura ya
taifa na kuonekana vyombo vya serikali vinashindwa kusimamia.
Jaji Mutungi amesema amani
ikiangaliwa kwa jicho la karibu kwa kutambua kuna maisha baada uchaguzi ambapo bila kufanya hivyo maisha
hayatakuwepo.
“Waandishi kwa kutumia kalamu zenu
mtafanya nchi ibaki kuwa na amani kwani wananchi wanaamini vyombo vya habari
kwa kila hatua inayotokea katika uchaguzi mkuu”amesema Mutungi.
Aidha amesema amevitaka vyama vya
siasa kutambua wajibu na sio kuangalia uchaguzi huru na haki kwani wajibu ndio
utafanya vitu view salama na kuweza kuvuka suala hili la uchaguzi mkuu.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Mstaafu,Francis Mutungi akizungumza mkutano wa wahariri na waandishi (hawapo pichani) juu ya amani kuelekea uchaguzi mkuu 25 ,uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wahariri na waandishi wa habari wakimsikilia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Mstaafu,Francis Murungi hayupo pichani katika mkutano wake uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wahariri na waandishi wa habari
wakiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Vyama Siasa nchini,Jaji Mstaafu
Francis Mutungi,jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...