Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini Kitabu cha Maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya Msiba iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.
Picha na OMR
Mola Mlaze pema peponi Amen. Imefanya nikumbuke enzi hizo tena miaka hiyo nikiwa shuleni katika kanda ya Ziwa, nakumbuka alikuja kupiga kampeni shuleni hapo, kama sijasahau ilikuwa ni kati yake Pascal Kulwa Mabiti & Paul Bomani na hapo ndipo nlipopata kumuona Marehem Mabiti. Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Mola awajaaliye faraja, subira na stahmala khususan katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa. Pumzika kwa amani Marehem Pascal Kulwa Mabiti - AMEN.
ReplyDeleteMay he rest in peace
ReplyDeleteMay he Rest in peace
ReplyDelete