Mzee wa heshima akielezea historia ya umiliki wa ardhi miaka ya nyuma ukilinganisha na sasa.
Makko
Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na
changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa
kupima mipaka katika vijiji husika.
Baadhi ya akina mama wa Kijiji hicho wakifuatilia tukio.
Na mwandishi wetu
Wenyekiti
wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za
kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa
mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la
Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT.
Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John
Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi
iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya
100 kutoka katika vijiji hivyo vinne.
Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha
Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru
mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi
na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi
kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na
kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi",
aliongezea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...