Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.
Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.
Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.
Picha na Dotto Mwaibale
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...