Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akiwanadi wagombea kiti cha Udiwani kwa wakazi wa Kinondoni kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
Dkt Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Ubungo Dkt Masaburi
Dkt Asharose Migiro akimwombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya TP,sinza jijini Dar.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Temeke,Ndugu Zuberi Abas Mtevu.
Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ubungo.Sinza jijini Dar kwenye uwanja wa TP wakati wa kampeni.Dkt Magufuli ameendelea na kampeni zake mkoani Dar es salaam,ambapo kesho ataendelea kuhutubia kwenye majimbo mbalimbali ya jiji hilo.

Mgombea huyo amefanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo na Kinondoni huku akiwanadi wagombea ubunge na udiwani wa majimbo hayo, Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika jumapili Oktoba 25 mwaka huu.
Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia CCM akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwasalimia baadhi ya wakazi wa mji wa Kigamboni,waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Machava Kigamboni leo.

PICHA NA MICHUZI JR-DAR ES SALAAM.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Chagua Magufuli aongeze uwajibikaji, Tanzania iende mbele kimaendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...