Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kweny mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi,

Katika mkutano huo wa hadhara Dkt.John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali atakayounda baada ya kuchaguliwa na Watanzania Oktoba 25 mwaka huu, itahakikisha inawatumikia huku akiweka wazi kuwa yeye  hakuwa na mchezo kwani dhamira yake ni kutatua shida za wananchi kwa spidi kubwa.

Amesema anatambua shida ambazo watanzania zinawakabili na hivyo uamuzi wake wa kuomba nafasi hiyo ni kuhakikisha anakabiliana nazo huku akisisitiza serikali yake,Mawaziri atakaoteua wajiandae kufanya kazi na atakayeona hawezi ni bora akajiweka pembeni mapema kabla ya kuapishwa ama akakataa uteuzi.

Dkt Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya wali0jinyakulia tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best Inspirational Song of The Year.

Wakati huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.

Dkt Magufuli amefanya kampeni zake katika jimbo la Nachingwea,Ruangwa,jimbo la Mtama na Lindi mjini huku akisimamishwa na wanachi mara kadhaa kila alikokuwa anapita.
Sehemu ya umati wa kazi wa mji wa Lindi Mjini wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura ya kuwania nafasi ya Urais.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akimuombea kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi jioni ya leo.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia mkutano wa kampeni a Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Lindi.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimuombea kura kwa wananchi Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtama,Ndugu Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mjumbea wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Mh Bernad Membe akiwahutubia wananchi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi mpili pili,mkoani Lindi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majaliwa,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi mara bada ya kumkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM.
Mmoja wa wafuasi wa chama cha CHADEMA akizungumza mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Ruangwa mara baada ya kurejesha kadi ya chama chake kwa Mgombea Urasi wa CCM Dkt Magufuli,ambapo wanachama wapatao 150 wa vyama mbalimbali pinzani walirejsha kadi zao.
Wananchi wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CCM tuko tayari awamu ya tano ni kazi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...