Bondia Thomas mashale wa manzese jijini Dar es salaam alifanya kitendo cha kusikitisha na kushangaza umma katika ukumbi wa friends corner uliopo Manzese ,pale alipomvamia katibu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe (bigright) kumpiga na kumpora simu na pesa. Akizungumza na vyanzo habari hizi Ibrahim kamwe alisema.”Nilikuwepo ukumbini  hapo friends corner nikishuhudia mpambano wa Jonas Segu na idd Pearali kwa kuwa watu walikuwepo ni wengi mno na pale mbele kulikuwa na fujo za ushangiliaji  nikaona ni bora nirudi nyuma kabisa ili nishuhudie kwa mbali , ghafla alitokea bondia huyo Thomas mashali akiwa na wenzake wanne akanishika mikono na wenzake kuanza kunisachi nilimputa mikono ili nizuie mifuko ndipo aliponipiga ngumi kali ya kidevuni na kichwani, watu walio karibu walipotugeukia sisi mashali na wenzake waliondoka haraka na kutokomea na simu yangu na kipochi  akiniacha na maumivu ya kidevu.

Nilichokifanya ni kuripoti polisi na kupewa PF3 na RB ili sheria ifuate mkondo wake.

Watu wengi waliokuwepo hapo ukumbini walisikitishwa na vitendo vya  bondia huyo kwa kuwa na matukio kama hayo mfululizo bila kujali anaowafanyia ni kina nani kwani hivi karibuni alimzuia kiongozi aliyekuwa akisafiri na bondia said mundi kuelekea nchini Thailand kwa kumshikia chupa na wenzake wakiwa na visu na kuwapora simu na pesa, bondia huyo wa tanga said mundi na Anthony ruta walikuwa wapole kwani tukio hilo alilifanya muda mchache kabla ya kuelekea airport.


Thomas mashali ni mwingi wa matukio kama hayo hasa maeneo ya manzese aliapa kujirekebisha kwa tabia hizo za ukabaji  lakini inaonekana amerudi kivingine sasa hata kwa watu anaowajua. Anafuatiliwa ili sheria ishike mkondo wakee 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duh! Huyo ni mwizi na sio bondia. Pole kwa wote waliopata madhara ya kichapo na kuibiwa. Ila asiachwe, sheria ifuate mkondo wake. Kama hawezi ngumu za mchezo arudi mtaani aendelee kukaba.

    ReplyDelete
  2. Huyu ni jambazi na anatumia ujuzi wake wa ngumi kwa njia ambayo siyo sahihi.

    Achukuliwe hatua haraka na akafungwe ili aende akapambane na mabingwa wenzake huko jela.

    ReplyDelete
  3. Mambo gani haya jamani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...