Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akimnadi Ole sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami kuunganisha na mikoa inayopakana na SImanjiro.Ole Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda Simanjiro.
Mbali na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.Twende na Magufuli popote alipo.Wananchi wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka huu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bila khofu kwa kata ya 'Kolo-Wasi' ondoa shaka, tuombe uhai na uzima hiyo siku ya siku In Sha Allah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...