
-Inaongoza katika sekta ya mawasiliano
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imepata
tuzo ya kuwa mwajiri bora katika sekta ya mawasiliano pia ipo miongoni mwa
makampuni kumi bora yanayotoa ajira na kuwa na mazingira bora kwa wafanyakazi
wake nchini Afrika ya Kusini kwa mwaka 2015.
Hafla ya kutangaza makampuni yanayoongoza
kwa ajira nchini Afrika ya Kusini ilifanyika jana katika eneo la Gallagher
Estate mjini Jahannesburg ambapo Vodacom ilitangazwa kuwa miongoni mwa
makampuni 10 bora yanayoongoza katika ajira na kwa kufuata taratibu na kanuni
za raslimali watu na ilitangazwa kuwa kampuni inayoongoza kwa kufuata misingi
bora ya ajira katika sekta ya mawasiliano.
Tuzo ya waajiri bora ni mpango ambao uandaliwa
kila mwaka na makampuni yanayoongoza kwa kufuata sheria na misingi bora ya
ajira na raslimali watu hutangazwa na kupewa tuzo.
Akiongea baada ya kupata tuzo hiyo Afisa
Mtendaji Mkuu wa raslimali watu wa Vodacom Matimba Mbungela alisema:”Tumewekeza
kwa kisi kikubwa katika uendeshaji wa shughuli za raslimali watu katika kampuni
yetu kuanzia teknolojia na kuweka mifumo bora inayokubalika kimataifa ambayo inatoa mwanya kwa wafanyakazi wetu
kufanya kazi katika mazingira mazuri na kampuni kuendesha shughuli zake kwa
ufanisi mkubwa”.
Mbungela alisema kuwa tuzo hii inatoa taswira halisi ya kampuni yetu kwa
kuwa kuwa mwajiri bora kunaendana sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja.
Tuzo hii imetolewa kwa Vodacom baada ya
kubainika kuwa inafuata na kutekeleza
kanuni na taratibu za raslimali watu zinazokubalika kimataifa na imekuwa mstari
wa mbele kuajiri wafanyakazi wazuri na kuendeleza vipaji vyao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...