
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU 38 KWA KUFANYA VURUGU NA UHARIBIFU WA MALI WILAYA YA MBOZI.
KATIKA
TUKIO LA KWANZA:
MNAMO
TAREHE 25.10.2015 KUANZIA MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HADI SAA 16:00 JIONI
KULIFANYIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WABUNGE
NA MADIWANI. KATIKA JIMBO LA RUNGWE, NDUGU SAUL H. AMON KWA TIKETI YA CCM NA
NDUGU JOHN MWAMBIGIJA KWA TIKETI YA CHADEMA NDIO WALIOKUWA WAKICHUANA VIKALI
KUGOMBEA KITI HICHO.
WAKATI
ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA KUFANYIKA KATIKA OFISI YA UCHAGUZI
JIMBO LA RUNGWE WATU WENGI NA KATIKA HAO WALIKUWEPO WAFUASI WA MGOMBEA UBUNGE
KWA TIKETI YA CHADEMA NDUGU JOHN MWAMBIGIJA
WALIKUSANYIKA NJE YA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE HUKU NA HAO
WAFUASI WA MWAMBIGIJA WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA DHIDI YA MGOMBEA WA
CCM, MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA JESHI LA POLISI AMBAO WALIKUWEPO PALE
KUHAKIKISHA KUNAKUWEPO HALI YA AMANI NA UTULIVU WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA
LIKIENDELEA.
ILIPOFIKA
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI WAFUASI HAO WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA AMBAO
ILIONEKANA WAMETOKA WALIOKUWA SEHEMU MBALIMBALI KAMA VILE RUNGWE, MBEYA MJINI,
TUNDUMA NA MAKETE WALIANZA KUFANYA FUJO NA VURUGU KWA KUWAZOMEA ASKARI NA
KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA MAWE, CHUPA NA FIMBO KWA MADAI YA KUTAKA MATOKEO
YATANGAZWE WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA.
KUFUATIA
VURUGU HIZO, JESHI LA POLISI LILIBIDI KUWATAWANYA WATU WALE KWA KUTUMIA MABOMU
YA MACHOZI NA KUPELEKEA WATU HAO KUTAWANYIKA NA KUANZA KWENDA MAENEO MBALIMBALI
NA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI ZA WATU KWANI WALICHOMA MOTO BAJAJI MOJA
ILIYOKUWEPO KARIBU NA ENEO LILE, KUVUNJA MADUKA YA WATU NA KUPORA MALI, KUCHOMA
MOTO MATAIRI KWENYE BARABARA YA LAMI, KUFUNGA BARABARA KUU ITOKAYO MBEYA KWENDA
KYELA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO YA MITI NA KUCHOMA MOTO HALI ILIYOPELEKEA
KUSABABISHA BUGHUDHA NA WATU NA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA.
JESHI
LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA DOLA, WALIFANYA OPERESHENI YA PAMOJA
ILI KUDHIBITI VITENDO VYA KIHALIFU VILIVYOKUWA VIKIFANYWA NA WAFUASI HAO AMBAO
WALIHAMIA MITAA MBALIMBALI. KUFUATIA OPERESHENI HIYO, WATU 158 WALIKAMATWA KUTOKANA NA MAKOSA HAYO YA KUFANYA
VURUGU/FUJO, KUCHOMA BARABARA, KUHARIBU MALI NA UPORAJI. JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO
VINGINE VYA DOLA – ASKARI WA JWTZ WALIFANIKIWA KURUDISHA HALI YA AMANI NA
KUIFANYA BARABARA HIYO KURUDI KATIKA HALI YA KAWAIDA NA MAGARI KUENDELEA NA
SAFARI.
WATUHUMIWA
WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE
27.10.2015 KUHUSIANA NA MAKOSA YA KUFANYA FUJO, VURUGU, KUCHOMA BARABARA
MOTO, UPORAJI NA KUSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI. PAMOJA NA KWAMBA WALIOKAMATWA
WAMESHAPELEKWA MAHAKAMANI, BADO TUNAENDELEA KUWATAFUTA WENGINE AMBAO BADO
HAWAJAKAMATWA ILI WAKAMATWE NA WAFIKISHWE MAHAKAMANI KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MNAMO
TAREHE 26.10.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA JIMBO LA
VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA WAKATI ZOEZI LA KUJUMLISHA MATOKEO YA
UBUNGE LINAENDELEA KUNDI LA VIJANA WANAOSADIKIWA KUWA NI WAFUASI WA CHADEMA
LILIJITOKEZA NA KULETA VURUGU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA KATA YA MLOWO KWA
MADAI YA KUSHINIKIZA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA VWAWA YATANGAZWE HARAKA.
KUFUATIA
MADAI HAYO, KUNDI HILO LA VIJANA LILIANZA KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA WA MALI NA
SAMANI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA JIMBO HILO NA KATA YA MLOWO. MIONGONI MWA
MALI ZILIZOHARIBIWA NI PAMOJA NA, GARI T.763 CPD AINA YA NISSAN YENYE THAMANI
YA TSHS. 85,000,000/= MALI YA GEORGE
EMMANUEL MKAZI WA MLOWO AMBALO LILICHOMWA MOTO.
OFISI
YA MTENDAJI KATA YA MLOWO ILIHARIBIWA NA SAMANI ZILIZOKUWEMO KUTEKETEZWA KWA
MOTO. THAMANI YA UHARIBIFU HUO INAKADIRIWA KUWA NI TSHS. 4,950,000/=. MAJIRA YA
SAA 20:00 USIKU WAFUASI HAO WA CHADEMA WALIMJERUHI DEOGRATIAS KAPESA (40) MKAZI WA MLOWO KWA KUTUMIA JIWE.
MAJIRA
YA SAA 20:20 USIKU GARI T.206 DCA
AINA YA RAV 4 LENYE THAMANI YA TSHS 13,000,000/= MALI YA TWEEDSMRY ZAMBI (61) LILICHOMWA MOTO NA KUHARIBIKA KABISA. GARI
HILO LINASADIKIWA MMILIKI WAKE NI NDUGU WA ALIYEKUWA MGOMBEA WA KITI CHA UBUNGE
KWA TIKETI YA CCM JIMBO LA MBOZI Mhe. GODFREY ZAMBI.
PIA
KATIKA VURUGU HIZO, PIKIPIKI YENYE NAMBA T.115
ACP MALI YA TWALIB MWANGA
ILICHOMWA MOTO NA WAFUASI HAO. THAMANI YA PIKIPIKI HIYO NI TSHS. 1,800,000/=.
WAFUASI HAO WALIFIKA KATIKA HOTEL YA CALIFONIA NA KUHARIBU MALI NA SAMANI ZA
JENGO HILO LA HOTELI KWA KUVUNJA MILANGO NA MADIRISHA YA JENGO HILO
YALIYOTENGENEZWA KWA ALUMINIUM NA KUFANYA UHARIBU KATIKA MAGARI MANNE
YALIYOKUWA YAMEEGESHWA NJE YA HOTEL HIYO. KATIKA UHARIBUFU HUO, MOJA YA GARI
YENYE NAMBA T.326 AINA YA TOYOTA
NOAH LENYE THAMANI YA TSHS. 16,500,000/= LILICHOMWA MOTO NA KUTEKETEZA VITU
VINGINE VILIVYOKUWEMO NDANI AMBAVYO NI US DOLLAR 2160 SAWA TSHS. 700,000/=
JUMLA YA THAMANI YOTE NI TSHS. 21,715,000/= MALI YA SUBIRA MBUBA (40) MKAZI WA
VWAWA. PIA WALICHOMA MOTO OFISI ZA CHAMA CHA CCM ZILIZOPO MLOWO NA VWAWA,
THAMANI YA UHARIBU HUO BADO KUFAHAMIKA. PIA WALICHOMA BARABARA KWA MAGOGO, MITI
NA MATAIRI KATIKA BARABARA YA LAMI ENEO LA MLOWO KUELEKEA VWAWA NA KUSABABISHA
UHARIBIFU WA BARABARA, MAGARI YANAYOPITA BARABARA HIYO NA USUMBUFU KWA
WATUMIAJI WA BARABARA HIYO.
KUTOKANA
NA VURUGU HIZO, JESHI LA POLISI LILIFIKA KATIKA MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA
KUREJESHA HALI YA AMANI, AIDHA JUMLA YA WATUHUMIWA 116 WALIKAMATWA, KATI YAO 78
WALIPELEKWA MAHAKAMA YA MKOA WA MBEYA KWA MAKOSA YA KUHARIBU MALI, KUHARIBU
KARATASI ZA KURA ZILIZOPIGWA PAMOJA NA MASANDUKU YAKE NA KUSABABISHA FUJO,
VURUGU NA UVUNJIFU WA AMANI. WATUHUMIWA 38
WALIFIKISHWA MAHAKAMA YA WILAYA – MBOZI KWA MAKOSA YA KUHARIBU MIUNDOMBINU
– BARABARA TAKRIBANI KILOMITA 20 KUTOKA MLOWO HADI VWAWA NA KOSA LA KUHARIBU
MALI NA KUFANYA VURUGU.
AIDHA
KATIKA VURUGU HIZO, ASKARI 06 WALIJERUHIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI KWA
KUPIGWA MAWE LAKINI WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI
WA MKOA WA MBEYA KUWA NA UTULIVU NA UVUMILIVU KATIKA MAMBO YANAYOHITAJI
TARATIBU ZA KISHERIA KUFANYIKA KATIKA KUHESABU KURA NA KIPINDI HIKI CHA KUTANGAZA
MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA KWA NAFASI MBALIMBALI KUANZIA UDIWANI, UBUNGE NA
URAIS. PIA WAEPUKE KUSHAWISHIWA KUFANYA VITENDO AMBAVYO NI KINYUME CHA SHERIA
LAKINI PIA NI KINYUME NA UTAMADUNI WA NCHI YETU KWANI WAO WANASHAWISHIWA NA
WATU WENGINE WAKATI WAO NDIO WANAOPATA MATATIZO. LAKINI PIA KWA KUVURUGA AMANI
NA UTULIVU KATIKA JAMII YETU NDIVYO TUNAVYOPELEKEA JAMII ZETU NA NCHI YETU KWA
UJUMLA KURUDI NYUMA KWENYE MAENDELEO YA
KIUCHUMI. PIA TUNAWAOMBA SANA WASISABABISHE JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU
KUPITA KIASI.
Imesainiwa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Waliofanya vurugu wachukuliwe hatua za kisheria. Hatutaki vurugu hapa au uharibifu wa mali yoyote kinyume cha sheria.
ReplyDelete